John Mnyika:Uzinduzi hospitali ya Sinza na ufafanuzi sahihi wa suala la Sekta ya Afya - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

John Mnyika:Uzinduzi hospitali ya Sinza na ufafanuzi sahihi wa suala la Sekta ya Afya

Mbunge wa Jimbo la Ubungo-(CHADEMA).John Mnyika
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mbunge wa Ubungo(CHADEMA) Mhe John Mnyika na kwa pamoja wakifungua rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sinza Palestine Kinondoni jijini Dar es salaam jana December 12, 2012
--
Jana, 11 Desemba 2012 Nimeshiriki uzinduzi makabidhiano ya jengo la huduma za mama na mtoto katika hospitali ya Sinza (ipo Sinza-Palestina) kwa msaada wa Korea ikiwa ni sehemu ya kuboresha huduma za afya.
Ipo haja ya kuongeza watumishi wa afya ikiwemo madaktari kwa kupanua wigo wa elimu kwa ujenzi wa Chuo Kikuu MUHAS, eneo la Kwembe Mloganzila.


Hata hivyo, nilitarajia Rais Kikwete angeeleza serikali ilivyojipanga kuboresha maslahi ya madaktari kwa kurejea taarifa ya kamati ya huduma za jamii iliyoundwa baada ya mgomo wa madaktari ili kuepusha kasi ya madaktari kwenda nchi za nje, badala yake Rais ametoa kauli nyingine tata.


Aida, Rais amepotoshwa kuwa wanasiasa wa upinzani wamepinga ujenzi wa MUHAS na kuahidi fidia ya usumbufu. Ukweli ni kuwa aliyewaahidi wananchi fidia ya ardhi ni aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Bwana John Chiligati mnamo mwaka 2009 na 2010 kwa ajili ya CCM kupata kura kwenye uchaguzi za serikali ya mitaa na Uchaguzi Mkuu. Wananchi wanachodai ni waliyoahidiwa na serikali.

John John Mnyika,
Mbunge wa Jimbo la Ubungo,
12/12/2012

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages