Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa (wa
kwanza kulia) akikagua mfumo wa maji taka katika Hotel ya Double Tree
jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Waziri ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais, Charles Kitwana na Dkt. Robert Ntakamulenga kutoka Baraza la
Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
…………………………………………………………………..
Lulu Mussa na Ali Meja
Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Dk. Terezya Huvisa hii leo ameifungia hotel ya Double Tree ya Jijini Dar es Salaam kutokana na kutiririsha maji taka baharini.
Waziri Huvisa ametoa agizo hilo
mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza akiwa na Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais Mheshimiwa Charles Kitwanga. Ziara hiyo ililenga kuona
utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa awali na Naibu Waziri Mh. Charles
Kitwanga mapema mwezi huu, alipofanya ziara kutembelea viwanda na hoteli
zilizo pembezoni mwa bahari kuona mfumo wa maji taka.
Katika ziara hiyo, Hotel ya Double Tree
iliagizwa kuwa na mpango wa muda mfupi na wa haraka wa kusitisha
utiririshaji wa maji taka baharini ambao mpaka leo hotel hiyo ilikuwa
bado haijatekeleza. Sambamba na hilo na hilo Waziri
Huvisa amefuta hati ya ukaguzi wa Mazingira (Environemental Audit) na
kuitaka hoteli hiyo kurekebisha mara moja mfumo huo ikiwa ni sambamba na
kulipa faini kwa baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)