Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) tayari
imemuandalia bondia, Francis Cheka, pambano la marudiano kati yake na bondia
Chiotra Chimwemwe wa Malawi katika jiji la Addis Ababa,
Ethiopia.
Mpambano
huo unatarajia kutafayika January 26, siku ya ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa nchi za Africa
(AU Summit) katika jiji hilo la Wafalme la Abesinia.
Cheka na
Chimwemwe, watakutana jijini Arusha Desemba 26 (Boxing Day) katika mpambano wa
kutafuta nani mbabe wa uzito wa Super Middle katika bara la Afrika, Mashariki ya
Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG). Katika mpambano huo mafahali hawa wawili
wataumana kiume kwa raundi 12 za dakika tatu kila mmoja!
Mpambano
wa Cheka na Chimwemwe jijini Arusha umeandaliwa na kampuni ya Screen Hills (T)
Investment ya jijini Dar-Es-Salaam inayomilikiwa na promota maarufu aliyewahi
kuwa bingwa wa taifa katika ngumi za ridhaa na kulipwa Andrew George aka Chagga
Boy!
Umaarufu wa wawili hawa umewafanya
mapromota wanaoandaa tamasha la kuchangisha pesa kwa ajili ya kulisha watu wenye
njaa katika bara la Africa kuwaingiza Cheka 26(15)-6(3)-1 na Chiotra
26(15)-4(2)-1 katika
mpambano hwa marudiano utakaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 26
Januaru 2012!
Katika
tamasha hilo, pambano kuu litakuwa kati ya bondia Oliver McCall 56(37)-12(1)-0
kutoka Marekani ambaye aliwahi kuwa bingwa wa uzito wa juu duniani akipambana na
bondia Sammy Retta - 18(17)-3(2)-0 kutoka Ethiopia kugombea ubingwa wa IBF
Africa, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa juu
(Heavyweight)
Mapambano mengine yatawakutanisha mabondia Daniel
Wanyonyi 14(12)-5(2)-2 wa Kenya atakayechuana na bondia Issac Hlatswayo
30(10)-5(3)-1 kutoka Afrika ya Kusini katika kugombea ubingwa wa IBF Afrika,
Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa
Welterweight
Naye
Manzur Ali 7(4)-8(3)-0 bingwa wa uzito wa juu kutoka nchi ya Misri atachuana
vikali na bondia Harry Simon 27(20)-0-0 kutoka Namibia ubingwa wa IBF Afrika,
Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa Light
heavyweight.
Mpambano
huu umeidhinishwa na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) na Cheka kupewa
kibali na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC).
Imetolewa na:
Onesmo A,M, Ngowi
Rais,
TPBC
Rais,
IBF /Africa
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)