Peer
Educators kutoka kampuni ya CFAO MOTORS Grasiano Mfuse (katikati) na
Maria Petro wakikabidhi Samani kwenye darasa la Watoto yatima la
Tanzania Mitindo House (TMH) ikiwa ni utaratibu wa Kampuni hiyo kila
mwaka Disemba Mosi wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani kutoa
misaada kwa vituo vya kulelea watoto yatima.Anayepokea msaada huo ni
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Kituo cha Watoto yatima wa Tanzania Mitindo
House (TMH) Bi. Khadija Mwanamboka.
Peer
Educators wa kampuni ya CFAO MOTORS Grasiano Mfuse (katikati) na Maria
Petro wakikabidhi msaada wa chakula, mafuta na maziwa kwa Mwenyekiti wa
TMH Bi. Khadija Mwanamboka kwa ajili ya watoto wa kituo cha Tanzania
Mitindo House ambao miongoni mwao wanaishi na Virusi vya Ukimwi.
Pichani
juu na chini ni Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Kituo cha Watoto yatima wa
Tanzania Mitindo House (TMH) Bi. Khadija Mwanamboka akitoa shukrani kwa
Ujumbe wa CFAO MOTORS kwa kutambua mchango wake katika jitihada zake za
kulea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Wanafunzi
na Ujumbe wa CFAO MOTORS ndani ya Chumba cha darasa la THM
kilichopambwa na kuwekwa Samani na Kampuni hiyo Ujumbe wa CFAO Motors
wakitizama ufanisi wa kazi za mikono zinazofanywa na watoto yatima wa
vituo mbalimbali waliokusanyika kupata mafunzo ya ufundi bure katika
shule ya Tanzania Mitindo House. Kulia Meneja Masoko wa CFAO MOTORS Bi.
Tharaia Ahmed na Peer Educators kutoka kampuni hiyo Bw. Grasiano Mfuse
(kushoto) na Maria Petro (katikati).
Mwalimu
wa Darasa la TMH la watoto yatima wa vituo mbalimbali la Tanzania
Mitindo House Dkt. Linda August akiwafundisha mabinti kutengeneza baadhi
ya bidhaa za urembo kama mikufu na hereni kwa kutumia shanga
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)