WIZARA ya Afya ya nchini Australia (GHAWA), kupitia Idara
ya Uuguzi na Ukunga imetoa gari mbili za kusafirisha wagonjwa
mahututi (Ambulance ), kwa mkoa wa Pwani wilayani Kisarawe.
“2011 wizara ilianza
kushirikiana na Australia hususani katika mambo muhimu ya afya kama
upanuzi wa vituo vya afya hususani kwa kuviboresha kutoka kwenye
hospitali za wilaya hadi mkoa, kwasababu serikali peke yake haiwezi
kulingana na ukubwa wa changamoto zake“ alisema Dk Regina.
Dk Regina aliongeza kuwa mbali
na msaada huo, wataangalia ujuzi wa Wauguzi katika vituo vya afya
nchini ili kubaini mapungufu yao na kuyaboresha.
Naye Mwakilishi kutoka
Australia Catherine Strodatt alitumia fursa hiyo kueleza kuwa nchi hiyo
itakuwa mstari wa mbele kushirikiana na Tanzania katika suala la afya.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)