KATIKA kuelekea sikuu za Krismasi na Mwaka mpya pilika pilika zimeongezeka katika mji wa Moshi na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla huku vibaka pia wakiendelea na udokozi na wizi wa vitu mbalimbali.
Mkazi wa kijiji cha Nshara Machame akivuja damu baada ya kupokea kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali kufuatia wizi wa mtoto wa Nguruwe,tukio hilo lilitokea juzi wilayani Hai.Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii - Moshi.
Katika kuthibitisha hilo juzi Tanzania Daima limeshuhudia mkazi wa kijiji cha Nshara, Machame wilayani Hai,ambaye jina lake halikupatikana mara moja amenusurika kuuawa kufuatia kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kumshambulia kwa silaha za jadi baada ya kuiba kitoto cha nguruwe maarufu kama "Kiti moto".
Tukio
hilo la aina yake ambalo linaashiria maandalizi ya siku kuu hizo
lilitokea juzi majira saa 5.30 asubuhi kijijini humo baada ya mkazi huyo
kuonekana akiwa amembeba mnyamya huyo begani akiwa katika mfuko,maarufu
kama Sandarusi mithili ya mzigo wa kawaida.
Akizungumzia
tukio hilo,mkazi wa kijiji cha Nshara, Husein Mbaruku alisema mtu huyo
alionekana akinyata katika banda la Nguruwe akiwa na mfuko wake akiamini
kuwa hakuna mtu aliyemuona ingawa wenyeji nao walikuwa wakimvizia ili
kuona anachotaka kufanya.
"Huyu
bwana ni mwizi mzoefu katika eneo hili ,mara kwa mara wenyeji hapa wamekuwa wakilalamika kuibiwa nguruwe wao leo naona Arobaini yake
imefika ,wananchi wamemkamata na ndio hivyo kama unavyoona kapigwa
sana"alisema Mbaruku.
Alisema
mtu huyo alifanikiwa kuiingia katika banda la nguruwe na kukikamata
mmoja ya kitoto cha nguruwe ambacho wakati wa harakati ya kuingizwa
katika mfuko huo kilipiga kelele ambazo ziliwashitua majirani wengine.
Kutokana
na mazingira hayo,mtuhumiwa huyo alikuwa mjasiri na kukimbia nacho
hivyo hivyo jambo lililosababisha baadhi ya wananchi kuanza kumfukuza
kwa kasi ndipo alipoanguka eneo la mfoni ambapo wananchi walimjeruhi kwa
silaha hizo ikiwamo mawe.
Katika hali isiyo ya kawaida huku mtuhumiwa huyo akivuja damu nyingine
mmoja wa raia alitaka kumchoma kwa gurudumu la gari ndipo wananchi
wenzake walipoingilia kati na kumuokoa mtuhumuwa huyo ambaye
alipelekwa kituo cha polisi bomangombe.
mmoja wa raia alitaka kumchoma kwa gurudumu la gari ndipo wananchi
wenzake walipoingilia kati na kumuokoa mtuhumuwa huyo ambaye
alipelekwa kituo cha polisi bomangombe.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)