Kalambo
Falls ambayo ni maporomoko makubwa ya maji ya asili yanayochukua nafasi
ya pili kwa ukubwa barani Africa yakiwa na urefu wa mita
235 yanapatikana Mkoani Rukwa mpakani na nchi jirani ya Zambia ni
miongoni mwa vivutio vya asili nchini Tanzania vyenye hadhi ya kupigiwa
kura kuwa miongoni mwa maajabu saba ya asili nchini Tanzania na barani
Afrika kwa ujumla. Vivutio vya Tanzania vinavyoshindanishwa na vingine
tisa (9) barani Afrika katika nafasi ya maajabu saba barani Afrika ni Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro na hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Pigia
vivutio hivi vitatu na vingine vinne ikiwemo Kalambo Falls kupata
vivutio 7 vya maajabu ya asili nchini Tanzania na barani Afrika.
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)