Meneja Huduma kwa wateja wa benki ya NMB Tawi la Bank House Steven
Chavala (mwenye Suti Nyeusi) akibonyeza kitufe kuwapata washindi wa promosheni ya Ki-College zaidi
na NMB. Kutoka (kushoto) ni Meneja Amana wa NMB, Boma Raballa, Meneja Masoko wa
NMB, Shilla Senkoro na Mkaguzi wa bodi ya michezo ya
kubahatisha ya Taifa, Humud Abdulhussein na Meneja bidhaa wa selcom, Julio
Batalio.
Meneja Masoko wa NMB, Shilla Senkoro akionesha zawadi ya taa ya kutumia mionzi ya jua
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Stephen Chavallah akibonyeza kitufe cha kompyuta kuwatafuta washindi wa promosheni hiyo.
Meneja
wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Stephen Chavallah (wa pili kulia)
akiangalia namna washindi wa promosheni ya Ki-College Zaidi na NMB
wanavyopatikana wakati wa droo ya kwanza iliyochezeshwa Makao Makuu ya
benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkaguzi wa Michezo ya
Kubahatisha, Humudi Abdulhussein. Kushoto ni Meneja wa Amana, Boma
Raballa na Meneja Masoko, Shilla Senkoro
..........................
Octoba 1, 2012 NMB
ilizindua promosheni ya Ki-COLLEGE zaidi na NMB inayowawezesha
wanafunzi wenye akaunti ya NMB Student Account kupata nafasi ya kuingia kwenye
droo na kujishindia zawadi mbalimbali kama: iPad, Samsung Galaxy, Amana
maradufu, flash disk, fulana za NMB, taa inayotumia mionzi ya jua. Hivyo basi,
wanafunzi waliofungua NMB Student Account, walioweka
amana katika akaunti zao au kujiungana NMB mobile wameweza kuingia kwenye droo
na wamepata nafasi ya kujishindia zawadi kwenye promosheni ya Ki COLLEGE
zaidi na NMB.
Katika droo ya kwanza ya Ki COLLEGE zaidi na NMB iliyochezeshwa
tarehe 12 Novemba, 2012, jumla ya washindi 66 walijishindia zawadi mbalimbali
kama ifuatavyo; Ipad 2, Samsung Galaxy 2, Amana
maradufu 2, taa inayotumia mionzi ya jua na jezi za timu ya Taifa 30.
Pamoja na kampeni hii, wanafunzi walioshinda na watakao fungua NMB
Student Account wataendelea kufurahia huduma za NMB Student Account kama: Kufungua
akaunti kwa Sh. 10,000 tu (pamoja na NMB ATM kadi),kujiunga na huduma ya NMB
mobile bure kupata huduma ya ujumbe mfupi kila utoapo fedha kwenye ATM ya NMB
bure, kuchukua fedha hadi Sh.1,000,000 kwenye NMB ATM kwa siku na kupata huduma
kupitia matawi zaidi ya 143 na NMB ATM zaidi ya 450 nchi nzima.
Ili uweze kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia zawadi
kwenye promosheni ya Ki COLLEGE zaidi na NMB, fungua NMB
Student Account, weka amana katika akaunti yako, tumia au jiunge na NMB mobile
.Ikiwa hujatumia akaunti yako kawa muda mrefu tembelea tawi la NMB ili nawe
ushiriki katika promosheni hii ya ki-COLLEGE
zaidi na NMB inayoendelea hadi Desemba 31, 2012.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)