Pages

Warembo watakaoziwakilisha Nchi za Rwanda na Kenya katika mashindano ya Miss East Africa mwaka huu wametangazwa rasmi

Mwakilishi wa Rwanda katika shundano la Miss East Afrika 2012
Mwakilishi wa Kenya katika shindano la Miss East Africa 2012.
.............................................................
Mrembo atakae iwakilisha Rwanda ni UMWARI NEEMA (22) ambae ana urefu wa futi 5.9 ambae ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo cha Kigali Institue of Education ( KIE) na pia ni mfanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo jijini Kigali.

Mrembo atakaeiwakilisha Nchi ya Kenya ni JOAN WAMBUI NDICHO (18) mwenye urefu wa futi 5.8 na anayetarajia kujiunga na Chuo kikuu cha Machakos University College kusomea mambo ya utalii

Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 mwezi December mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.

Mashindano ya Mwaka huu yanayosubiliwa kwa hamu yanatarajiwa kushuhudiwa na mamilioni ya watu Duniani kupitia kwenye luninga zao na pia kwa njia ya Internet ambapo yatautangaza utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa na pia kujenga umoja wa Afrika mashariki na kudumisha utamaduni wa ukanda huu wa Afrika.

Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)