Pages

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amtembelea Kepteni mstaafu wa meli za Serikali Kepteni Abdalla Said Abeid

   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na vijana wa Mji Mkongwe wakati akirudi kumtembelea Kempeni Mstaafu wa meli za Serikali Abdalla Said Abeid nyumbani kwake Malindi mjini Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na Kepteni Mstaafu wa meli za Serikali Abdalla Said Abeid nyumbani kwake Malindi mjini Zanzibar, alipokwenda kumtembelea na kumjuilia hali.Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
--
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amefanya ziara ya kumtembelea Kepteni mstaafu wa meli za Serikali Kepteni Abdalla Said Abeid ambaye amekuwa akisumbuliwa na maradhi mbali mbali kwa kipindi kirefu sasa.
 
Kepteni Abeid mwenye umri wa miaka 71 mkaazi wa Malindi Mjini Zanzibar amekuwa akisumbuliwa na maradhi tofauti yakiwemo matatizo ya magoti.

Katika maelezo yake Kepteni Abeid amesema kwa sasa hali yake inaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu katika hospitali tofauti nchini na baadaye nchini India.
 
Makamu wa Kwanza wa Rais amemuombea kepteni huyo mstaafu apone haraka ili ameweze kujumuika na wanajamii na taifa kwa jumla katika harakati za maendeleo.
 
Maalim Seif amekuwa akifanya ziara za mara kwa mara za kuwatembelea wagonjwa pamoja na wazee katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba.


Na 
Hassan Hamad 
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)