WADAU WA ELIMU CHATO WALALAMIKIA ELIMU YA AWALI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

WADAU WA ELIMU CHATO WALALAMIKIA ELIMU YA AWALI

Watoto wa awali wa shule ya msingi Kalema.
 Watoto wa awali wa shue ya msingi Chato.
-
Na Daniel Limbe,Chato

LICHA ya serikali kuhamasisha uanzishwaji wa elimu ya awali katika shule zote za msingi hapa nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kimaarifa watoto ambao hawajafikia umri wa kuanza elimu ya msingi,hatua hiyo imeonekana kulalamikiwa sana na baadhi ya wadau wa elimu katika wilaya ya chato mkoani geita kutokana na kukosekana kwa miundo mbinu mbalimbali ya kufundishia.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi baadhi ya walimu wakuu wa shule za msingi Kalema,Kitela na Chato wamesema upatikanaji wa elimu ya awali kwa watoto ni changamoto kubwa kwa serikali kutokana na ukosefu mkubwa wa vitabu vya kufundishia,vifaa vya kujifunzia na uhaba wa walimu.

Kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chato Mwita Chacha shule yake inawanafunzi wa awali 300 na kwamba watoto hao wanamwalimu mmoja na kwamba hakuna madawati ya kukalia wala vifaa vya kujifunzia kwa vitendo hali inayosababisha watoto wengi kushindwa kupata elimu iliyokusudiwa.

Amesema kitendo cha mwalimu mmoja kufundisha watoto 300 hakiendani na mpango wa kitaifa wa utoaji elimu ambao unamtaka mwalimu mmoja kufundisha watoto 40 huku akiiomba serikali kuimalisha miundombinu ya kufundishia itakayosaidia kuboresha elimu kwa watoto wa shule za awali.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kalema Tano Bara amesema ili elimu ya awali iweze kupatikana kwa ufanisi kuna haja kubwa kwa serikali kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya kununua vitendea kazi vya kufundishia na kufundishiwa hatua itakayorahisisha upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wa awali ikilinganishwa na hali ilivyo hivi sasa.

Aidha uchunguzi wa Mwandishi wa habari hizi umebaini aslimia 95 ya shule za awali wilayani chato hakuna vitabu vya kufundishia watoto badala yake walimu wa madarasa hayo hulazimika kutumia mihutasari inayotoa miongozo ya kutolea elimu hiyo huku madawati na vifaa vingine vya kujifunzia vikionekana kitendawili.

Kutokana na hali hiyo baadhi ya watoto wa awali imeonekana ni vigumu kwao kujifunza kwa ufasaha kutokana na baadhi yao kukaa chini na wengine kukalia mawe wakati wa kujifunza hivyo kusabisha watoto kuwa na miandiko isiyofaa.

Alipotakiwa kujibu malalamiko hayo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chato Shaban Ntarambe alidai kuwa yeye siyo msemaji licha ya kudai kuwa serikali inayafahamu mapungufu yaliyopo na kwamba taratibu bado zinafanyika ili kutatua hali hiyo.

Aidha amedai kuwa mwongozo alionao unamuelekeza kusimamia uandikishwaji wa watoto wa shule za awali kila kijiji na kwamba hatua zingine zitafuatwa kulingana na mpango wa serikali.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages