Mwezeshaji
katika mafunzo ya Ujasiriamali katika Wiki ya Ujasiriamali Duniani
Austin Makani (kushoto) akitambulisha meza kuu wakati wa Hafla ya
kukabidhi vyeti kwa wahitimu na kufunga Mafunzo hayo. Mgeni rasmi Mkuu
wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Ulingeta
Mbamba (katikati), Mratibu Mipango wa Kitengo cha Ujasiriamali cha Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDEC) Bw. Elia Yobu (kulia), Makamu Mwenyekiti
wa ZAYEE Bw. Omar Said Shabaan (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa
Professional Approach Development Bi. Lillian Secelela Madeje (kushoto)
na Katibu Mkuu wa Shirika Lisilo la Kiserikali
la ZAYEE (Zanzibar Association for Youth Education and Empowerment)
Fatma Mabrouk Khamis (wa pili kushoto).
Pichani Juu na Chini ni Mkuu
wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Ulingeta
Mbamba akitoa hotuba wakati wa kufunga mafunzo ya Ujasiriamali kwa
Vijana yaliyoandaliwa na Asasi ya ZAYEE (Zanzibar Association for Youth
Education and Empowerment) na kutolewa na Kitengo cha Ujasiriamali cha
Chuo Kikuu cha DSM (UDEC).
Dkt.
Mbamba amesema mafunzo hayo ni muhimu sana kwa vijana kwa kuwa
yatawawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi, umahiri, tija zaidi na
yatawasaidia sana katika kufanya shughuli zao za kila siku ziwe za
kujiajiri wenyewe au kuajiriwa.
Katika
mafunzo hayo jumla ya vijana 103 (68 kutoka Dar es Salaam na 35 kutoka
Zanzibar) wamejifunza mambo mengi pamoja na Ujasiriamali, Fursa za
Biashara zilizopo na Changamoto zake, Jinsi ya kupata Wazo la Biashara
pamoja na Mpango wa Biashara.
Katibu Mkuu wa ZAYEE Bi. Fatma Mabrouk Khamis akiwapa nasaha wakufunzi
wa mafunzo ya Ujasiriamali na kuwataka elimu waliyoipata hapo ikazae
matunda katika kazi na biashara wanazozifanya ili kuongeza tija
itakayosaidia kukuza uchumi binafsi wa Taifa.
Pia ameahidi kuwafikia vijana wa Mikoani kuwapa mafunzo ya Ujasiriamali yatakayowezesha kuimarisha biashara zao.
Mwenyekiti
wa Shirika Lisilo la Kiserikali la ZAYEE (Zanzibar Association for
Youth Education and Empowerment) Bw. Masoud Salim Mohamed akizungumza na
wahitimu hao ambapo ametoa fursa kadhaa na kuwataka kujijengea
utamaduni wa kujiendeleza.
Mkurugenzi
Mkuu wa Professional Approach Development Bi. Lillian Secelela Madeje
akizungumzia umuhimu wa wajasiriamali kutumia michanganuo ya biashara
katika kukuza biashara zao.
Katibu Mkuu wa ZAYEE Bi. Fatma Mabrouk Khamis akipokea cheti kufuzu
mafunzo ya ujasiriamali wakati wa wiki ya Ujasiriamali Duniani kutoka
kwa Dkt. Mbamba ambayo kwa Tanzania ndio mara ya kwanza kufanyika.
Pichani Juu na Chini baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo yaliyomalizika jana jijini Dar es Salaam.
Meneja
Maendeleo ya Biashara wa Kibo Palace Hotel Charity Githinji (kulia)
akibadilishana mawazo na baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya Ujasiriamali
jinsi ya kupata wazo la biashara.
Wahitimu wa Global Entreprenuership Week Tanzania katika picha kumbukumbu pamoja na mgeni rasmi pamoja na wawezeshaji.
Bi. Fatma Mabrouk Khamis (wa pili kushoto) na Mwakilishi kutoka ILO pamoja na baadhi ya wahitimu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)