TAARIFA KWA UMMA
Uzinduzi wa Shindano la Kusaka Mabingwa wa Kero kwa Wateja
Jumuiya
ya watumiaji wa huduma mbalimbali nchini kupitia mitandao ya kijamii ya
Facebook na Twitter imezindua rasmi shindano la kusaka kampuni
zinazotoa huduma na bidhaa mbovu kwa wateja nchini Tanzania.
Jumuiya
hiyo inawajumuisha watu wa kada mbalimbali wakiwemo wanasheria,
wanaharakati, waandishi wa habari, viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara
na wateja wa huduma na bidhaa mbalimbali nchini Tanzania.
Lengo
la jumuiya hiyo ni kushinikiza wafanyabiashara nchini kutoa huduma na
bidhaa bora kwa wateja na kuwakumbusha umuhimu wa wateja. Kauli mbiu ya
wanajumuiya hao ni Mteja ni Mfalme.
Katika
wiki ya kwanza tangu jumuiya hiyo kuzinduliwa jumla ya makampuni 21
yameingizwa katika shindano hilo kwa wateja wao kuwasilisha malalamiko
yao. Kwa taarifa zaidi kuhusu ni fuatilia akaunti ya Twitter @hudumambayatz au kundi la Facebook linalojulikana kama HUDUMA BONGO.
Ili
kuweza kupiga kura yako unahitajika kuwa na akaunti hai (yenye
mawasiliano mara kwa mara) katika mtandao wa Twitter au Facebook na
kujiunga na jumuiya hiyo. Mara tu utakapowasilisha kero yako utaifanya
kampuni unayoilalamikia kuingia katika mchuano mkali wa kumsaka bingwa
wa huduma mbovu kwa wateja nchini.
Huduma
Bongo inatoa wito kwa makampuni yote kuboresha huduma na bidhaa zao ili
kuweza kuwapatia wateja kilicho bora zaidi katika soko hili la
ushindani.
Imetolewa na Mshauri wa Habari wa Huduma Bongo - hudumabongo@gmail.com
Novemba 9, 2012
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)