Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon kwa pamoja na Rais wa Baraza Kuu
la 67 la Umoja wa Mataifa, Bw. Vuk Jeremic, na Rais wa Baraza Kuu la
Usalama kwa mwezi wa Novemba, Balozi wa India, Hardeep Singh Puri
wakiwasha mishumaa, ikiwa ni ishara ya kuwaenzi na kuwakumbuka raia,
wanajeshi na polisi 29 ambao wamepoteza maisha katika kipindi cha
kuanzia Novemba 2011 hadi Agosti 2012 wakati wakitekeleza majukumu ya
ulinzi wa Amani katika Misheni 11 za Kulinda Amani za Umoja wa Mataifa.
Miongoni mwa marehemu hao waliokumbukwa katika hafla hiyo wapo wanajeshi
watatu kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) ambao ni Koplo
Yusuf Said Chinguile, Staff Sajenti, Julius Chacha Marasi na Private
Anthony Daniel Paul waliokuwa wakihudumu katika Jimbo la Darfur.
Baadhi ya
wageni wakiwamo mabalozi na Waambata jeshi wakifuatilia hafla maalum ya
kuwaenzi na kuwakumbuka raia, wanajeshi na polisi 29 waliopoteza maisha
katika kipindi cha kuanzia Novemba 2011 hadi Agosti 2012. Hafla hiyo
imefanyika siku ya Jumatano hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,
wengine waliopoteza maisha katika kipindi hicho wanatoka, Nigeria,
Kenya, Rwanda, India, Ethiopia, Niger, Jordan, Syria, Bangladesh, Sierra
leone, Senegal, Brazil, Afghanistan, Togo, Egypt.
Na Mwandishi Maalum
Umoja wa
Mataifa jana jumatano umefanya hafla maalum ya kuwaenzi na kuwakumbuka
wanajeshi, polisi na raia ambao wamepoteza maisha wakati wakitekeleza
jukumu la kulinda Amani chini ya Mwamvuli wa Umoja wa Mataifa.
Hafla
hiyo iliyojaa simanzi ya aina yake huku ikisindikizwa na nyimbo za
maombelezo kutoka kwaya maalum, iliwahusu jumla ya wahanga 29 kati yao
wakiwamo watanzania watatu ambao walikuwa Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi
la Tanzania ( JWTZ).
Wanajeshi
hao walikuwa wakihudumu katika kikosi cha Tanzania kilichoko katika
jimbo la Darfur nchini Sudan, chini ya Jeshi la Pamoja la Umoja wa
Mataifa na Umoja wa Afrika maarufu kama UNAMID.
Marehemu
Koplo Yusuf Said Chinguile, Staff Sajent Julius Chacha Marasi na Private
Anthony Daniel Paul walipoteza maisha kati kati ya mwaka huu.
Mbali ya
Wanajeshi hao kutoka Tanzania, nchi nyingine ambazo zimepoteza
wapiganaji wao katika kipindi cha kuanzia Novemba 2011 hadi Agosti 2012,
na idadi ya marehemu kwenye mabano ni Nigeria (5), Togo(1), Sierra
Leone(1),
Rwanda(1),Kenya(1),India(2),Jordan(1),Egypty(1),Ethiopia(1),Niger(7),Afghanistan(1),
Senegal(1) , Syria(1), Brazil(1) na Bangladesh(1).
Katika
salamu zake mara baada ya tukio la kuwasha mishuma ikiwa ni ishara ya
kuwakumbuka na kuwaombea pumziko la milele marehemu hao, Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa alikuwa na haya ya kusema.
“ Leo hii
tunawakumbuka wenzetu 29, raia, wanajeshi na polisi ambao wamepoteza
maisha katika misheni 11 walikokuwa wakihudumu. Wenzetu hawa
wanawakilishi mataifa 16. Kwa kupitia majina yao na historia yao,
tunauona Umoja wa Mataifa, hawa wametoka kila pembe ya dunia, hawa kuwa
na makuu, walijitolea kwa moyo wote kutekeleza jukumu hili mbali na nchi
zao. Baadhi yao wanatoka katika maeneo ambayo yamegubikiwa na
machafuko. Na walikuwa wamedhamiria kuleta amani kwa watu wengine”.
“
Tunakumbuka heshima ya kufanya kazi na wenzetu hawa, tunajivunia uamuzi
na dhamana waliyoichukua kufanya kazi katika Umoja wa Mataifa.
Tunaombeleza pamoja na familia zao na rafiki zao huku tukienzi uwezo wa
kila mmoja wao na mchango walioutoa kwenye kazi zetu na kwa dunia yetu.
Tafadhli ninawaomba muungane nami kwa dakika mmoja kuwakumbuka ndugu
zetu na rafiki zetu”. Akasema Ban Ki Moon, Katibu Mkuu wa Umoja huo.
Akabainisha
kwamba, vifo hivyo havikupashwa kutokea, lakini ni kielelezo dhahiri
cha mazingira magumu na ya hatari wanayokabiliana nayo wale wote
wanaojitolea kuhudumu katika Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa
Mataifa.
“Matumaini
yangu ni kutokokea kwa matukio kama haya ambayo si ya lazima, kwamba
watu wetu wote waweza kutekeleza majukumu yao bila ya kuhatarisha maisha
yao. Lakini, tunatambua wazi kwamba Operesheni za kulinda Amani za
Umoja wa Mataifga na watu wote wanaohudumu katika operesheni hizo,
wamekuwa wakikabiriwa na mazingira hatarishi kwa usalama wao” akasema
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Na Kuongeza “ Na wapumzike kwa amani, wakati tukiendeleza yale waliyokuwa wakiyafanya”.
Baada ya
salamu za Katibu Mkuu pamoja na zile ziliyotolewa na Rais wa Baraza la
67 la Umoja wa Mataifa Bw, Vuk Jeremic , Rais wa Baraza Kuu la Usalama
kwa mwezi huu wa Novemba, Balozi wa India, Hardeep Sing Puri ns Bi
Paulina Analea Mwakilishi wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, kulifuatia
tukio la kusomwa kwa jina moja baada ya jingine la marehemu hao 29.
Hafla hiyo ilihitimishwa kwa wimbo mwingine wa maombolezo “ The Lord Bless You and Keep You”.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)