Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad
akisalimiana na ujumbe wa wanafunzi wa chuo cha ulinzi cha Taifa cha
Tanzania waliofika ofisini kwake Migombani. Katikati ni kiongozi wa
ujumbe huo Brigedia Jenerali JM Mwaseba.
Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipokea zawadi kutoka kwa
kiongozi wa ujumbe wa wananchi wa chuo cha ulinzi cha Taifa huo Brigedia
Jenerali JM Mwaseba
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiwa
katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chuo cha ulinzi cha Taifa
Tanzania waliofika ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar.Picha na
Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
----
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema suala la
amani na usalama ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya nchi na watu wake.
Amesema
suala hilo linapaswa kuzingatiwa na kufanyiwa kazi ili kuhakikisha kuwa
amani ya Tanzania inaendelea kuwepo wakati wote kwa lengo la kuendeleza
sifa ya Tanzania kiusalama, sambamba na kukuza uchumi wa nchi.
Maalim
Seif ametoa changamoto hiyo leo ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar
alipokuwa na mazungumzo na ujumbe wa wanafunzi wa chuo cha ulinzi cha
Taifa Tanzania (National Defence Collage) cha Dar es Salaam, waliofika
ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha na kubadilishana mawazo.
“kulinda amani ya nchi yetu ni suala muhimu sana kwa maendeleo ya taifa
ya taifa letu, na nachukua nafasi hii kuipongeza Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kwa kuanzisha chuo hichi”,alieleza.
Amesema
nchi zilizoendelea na zina zinazoendelea kwa kasi zilianza kazi ya
kulinda usalama wa nchi zao kwa kipindi kirefu, na ndio maana ziliweza
kupata mafanikio katika Nyanja mbali mbali za kiuchumi na kijamii. Amesema
ni vyema vyombo vya ulinzi na usalama kuanza kudhibiti viasharia vya
uvunjifu wa amani mara vinapogungudua hali hiyo, ili kuiepusha nchi
kuingia katika janga la uvunjifu wa amani.
Aidha
amesema katika kukabiliana na vitendo vya uvunjifu wa amani serikali
inapaswa kujipanga kukabiliana na kero za wananchi hasa ukosefu wa ajira
kwa vijana.
Makamu
wa Kwanza wa Rais amefahamisha kuwa vijana wengi ambao wamehitimu
masomo katika fani mbali mbali bado hawana ajira na kwamba hali hiyo
inaweza ikawapelekea vijana hao kufanya vitendo visivyokubalika katika
jamii.
Kwa
upande wake kiongozi wa ujumbe huo Brigedia Jenerali JM Mwaseba
ameelezea matumaini yake kuwa wahitimu wa chuo hicho wataweza kuongeza
ujuzi wao katika masuala ya ulinzi na usalama na kusaidia mabambano
dhidi ya vitisho na vitendo vya uvunjifu wa amani.
Amefahamisha
kuwa wahitimu wa chuo hicho pia watakuwa ni watunga sera wazuri katika
taasisi wanazotoka, lengo likiwa ni kuimarisha hali ya usalama na
kuimarisha uchumi wa nchi.
Jenerali
Mwaseba ameongeza kuwa kozi hiyo ya mwaka mmoja kwa kuanzia
imewashirikisha wanafunzi wa Tanzania pekee kutoka taasisi mbali mbali
za serikali Muungano na Zanzibar wakiwemo watendaji kutoka Jeshi la
Wananchi, Jeshi la Polisi na Taasisi za kiraia.
Na
Hassan Hamad
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)