tgnp yaadhimisha muendelezo wa SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA duniani - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

tgnp yaadhimisha muendelezo wa SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA duniani


Muwakilishi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii,Dkt. Grace Mallya akizungumza mapema jana kwenye maadhimisho ya muendelezo wa Siku 16 za Kupinga Ukatili wa kijinsia,zilizofanyika kwenye viwanja vya Mtando wa Jinsia Tanzania (TGNP),Mabibo jijini Dar Es Salaam.Chimbuko la Siku 16 za kupinga Ukatili  wa Kijinsia ni mauaji ya kinyama ya wadada wa Mirabelle yaliyofanyika nchini Dominika mwaka 1960. Kuanzia Novemba 25 mwaka 1991, Umoja wa Mataifa uliitenga siku hii kama Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake. 

Maadhimisho haya yanafikia kilele tarehe 10 Desemba ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Kuadhimisha Tamko Rasmi la Haki  za Binadamu, ikiwa ni ishara ya kuhusisha ukatili dhidi ya wanawake na haki za binadamu na vile vile kutia msisitizo kwamba ukatili kama huu ni uvunjwaji wa haki za binadamu. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),Bi.Usu Mallya na shoto ni Muwakilishi kutoka shirika la UNFPA,Anna Holmstrom.
Muwakilishi kutoka shirika la UNFPA,Anna Holmstrom nae akichangia mada mbalimbali zilizotolewa kwenye maadhimisho ya muendelezo wa Siku 16 za Kupinga Ukatili wa kijinsia,zilizofanyika kwenye viwanja vya Mtando wa Jinsia Tanzania (TGNP),Mabibo jijini Dar Es Salaam jana.Chimbuko la Siku 16 za kupinga Ukatili  wa Kijinsia ni mauaji ya kinyama ya wadada wa Mirabelle yaliyofanyika nchini Dominika mwaka 1960.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),Bi.Usu Mallya akizungumza mapema jana mchana kwenye maadhimisho ya muendelezo wa Siku 16 za Kupinga Ukatili wa  kijinsia,zilizofanyika kwenye viwanja vya Mtando wa Jinsia Tanzania (TGNP),Mabibo jijini Dar Es Salaam.Siku hizi 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia zimekuwa zikitumika na wadau ulimwenguni kote kama mbinu mahsusi za kutoa wito kwa jamii ili kumaliza aina  zote za ukatili wa kijinsia kwa kufanya yafuatayo:-• Kujenga uelewa kuhusu ukatili wa kijinsia kama uvunjwaji wa haki za binadamu kijamii, kitaifa, kikanda na kimataifa. • Kuimarisha kazi za kupinga ukatili wa kijinsia katika ngazi za chini na kujenga daraja kati ya kazi za maeneo mbalimbali yanayoshughulikia ukatili dhidi ya wanawake. • Njia ya kubadilishana taarifa na uzoefu katika kuzuia na kupambana na  ukatili dhidi ya wanawake kati ya wadau. • Njia ya kuonyesha mshikamano ulimwenguni kote kupinga ukatili wa kijinsia. • Kama chombo cha kutumia kupaza sauti  ili wadau wote waweze kutekeleza wajibu wao katika kupiga vita ukatili  wa kijinsia. Kila mwaka kumekuwa na kauli mbiu kuhusiana na ukatili dhidi ya  wanawake. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “FUNGUKA: KEMEA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE. SOTE TUWAJIBIKE”.

 Baaadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho hayo wakifuatilia jambo 
 Igizo lenye mafunzo ya kupambana na kuondoa ukatili wa kjinsia likifanyika.
 Baadhi ya wafunzi walioshiriki maadhimisho hayo wakiimba
 Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia jambo kwenye maadhimisho hayo
Mmoja wa wafanyakazi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania,Dada Lilian Liundi akifafanua jambo kwa wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye maadhimisho hayo ya maadhimisho ya muendelezo wa Siku 16 za Kupinga Ukatili wa  kijinsia,zilizofanyika kwenye viwanja vya Mtando wa Jinsia Tanzania (TGNP),Mabibo jijini Dar Es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages