Waziri wa Uchukuzi Tanzania, Mheshimiwa Dr.
Harrison G. Mwakyembe- (Mbunge), akihutubia kwenye Mkutano Mkuu wa
Mwaka wa Jumuiya ya Waingereza waliowahi kuishi nchini Tanzania (Britain
Tanzania Society(BTS)). Mheshimiwa Waziri Mwakyembe alikuwa mgeni rasmi
katika Mkutano huo wa Mwaka wa Taasisi hiyo ya BTS yenye kutoa misaada
mingi kwa Tanzania, kama vile Vifaa vya kusomea, Ujenzi wa Shule, Vifaa
vya Mahospitalini, uchimbaji wa Visima na kusaidia upatikanaji wa maji
safi,misaada ya Kitaalam kwa Tanzania kwa ujumla.
Watanzania na baadhi ya Wanachama wa Jumuiya ya BTS,
wakizikiliza kwa Makini Hotuba iliyokuwa ikitolewa na mgeni rasmi
Mheshimiwa Waziri Dr. Harrison Mwakyembe kwenye Mkutano mkuu wa Mwaka,
siku ya jumamosi 10 Novemba 2012
Mheshimiwa Waziri Mwakyembe, Mheshimiwa Balozi wa
Tanzania, London (Mhe. Peter Kallaghe), wakiwa kwenye picha ya pamoja na
baadhi ya Watanzania waliohudhuria kwenye mkutano wa Jumuiya ya BTS,
siku ya jumamosi, terehe 10 Nov 2012, kwenye Ukumbi wa Westminster City
Hall, London.Picha na Habari na Mr. A. Rashid Dilunga ICT - Manager-Tanzania High Commission to London
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)