SUMATRA KUWAKAMATA WATAKAOPANDISHA NAULI ZA MABASI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SUMATRA KUWAKAMATA WATAKAOPANDISHA NAULI ZA MABASI

DAR ES SALAAMJ, Tanzania

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), imesema itawakamata wamiliki wa magari wote watakaohusika katika kupandisha nauli hovyo hvyo.

Msemaji wa Mamlaka hiyo, David Mziray amesema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati alipokuwa akizungumzia taarifa kuwa kuna baadhi ya madereva na makondakta kupandisha nauli kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

Alisema wamejipanga vizuri kwani wamewaandaa vijana watakaoshirikiana na Jeshi la Polisi ili kuzikamata kampuni za mabasi ambazo zitabainika kupandisha nauli kinyume cha sheria.

 Mziray alisema katika kipindi hiki wataendesha opresheni kila siku ya kukamata kampuni ambazo zitaenda kinyume na mkataba wao wa  leseni, itatozwa fani ya  sh 25000.

Sambamba na hilo, aliwatahadhalisha wamiliki wa magari hayo kuwa makini ili kuepuka kutozwa faini ambazo kwa kiasi kikubwa zinaumiza wao na wala siyo madereva na makondakta.

“Nafahamu kweli kuna baadhi ya magari hivi sasa yamekwishaanza kupandisha nauli kutokana na kuongezeka kwa abiria wanaosafiri kwenda kuungana na familia zao katika kipindi cha kusherehekea Sikukuu ya X-mas”alisema.

Mziray alisema SUMATRA haitasita kuzifutia leseni kampuni ambazo zitaonekana kuwa sugu katika kujiingiza kwenye vitendo hivyo vya kupandisha nauli kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kuwaibia wananchi.

Vile vile aliwaasa abiria  kutoa ushirikiano katika operesheni hiyo ya kuzikamata kampuni zinazojihusisha na upandishaji huo wa nauli, wakati mwingine wanashindwa kutekeleza majukumu yao kutokana na abiria wenyewe kuwa wagumu kuwafichua madereva na makondakta wanaofanya hivyo.

Hata hivyo,  Mziray alitoa wito kwa wananchi kupanga nasafari zao kwa utaratibu na wala siyo kurupuka kwani mara nyingi wale wanao kurupuka kwa kutaka kusafiri siku hiyo hiyo ndiyo maranyingi wanaokumbana na ubabaishaji huo katika kupata tiketi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages