Semina hiyo inalenga kutoa elimu
na hamasa kwa vijana juu ya namna ya kuingia katika soko la biashara na
kunufaika na fursa zilizoko katika soko hilo zitakazowawezesha
kujikomboa kiuchumi na kuachana na utegemezi hasa wakutegemea kuajiriwa.
Billy Mushi ni Mjasiriamali ambaye
ni mtoa mada anaeleza kuwa mafunzo hayo yamesaidia kuingiza watu wapya
kwenye biashara hususani watu wa ngazi mbali mbali kutoka
vyuoni,mashirika na benki na kuongeza kuwa vijana wanapaswa kujua kwamba
wananaweza kufanikiwa endapo watatumia mbinu za kijasiriamali.
Tayari wameshatoa elimu hiyo kwa
watu 1200 ambapo wanatoa mafunzo hayo si tu wale wenye uwezo wa
kufundisha tu bali ni watu wenye uzoefu na waliobobea katika soko la
biashara hivyo wanafunisha njia walizopitia ili kutoa hamasa kwa wengine
kuthubutu kutumia fursa za kibiashara zilizoko kwenye maeneo yao ili
waweze kufanikiwa kiuchumi,kimaisha na kutimiza ndoto zao.
Hata hivyo ametoa wito kwa vijana
kushiriki katika semina,warsha mbali mbali na mafunzo ya ujasiriamali
ili kujijengea uwezo,maarifa na mbinu za kufanikiwa kiuchumi ili
kuondokana na umasikini,utegemezi na tatizo sugu la ukosefu wa ajira
linalowakabili vijana wengi nchini.
Joseph Mayagila ni Mkurugenzi wa
Mafunzo katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha (AJTC)
kilichoshiriki katika mafunzo hayo anasema kuwa mafunzo hayo hayawaandaa
wanafunzi kutegemea mshahara tu bali yaawaandaa kufanikiwa kiuchumi
aidi ya hapo ili mwanafunzi anapohitimu chuo aweze kujimudu kiuchumi
mbali na kutegemea ajira peke yake.
Mkurugenzi huyo aliendelea kusema
kuwa mafunzo hayo yatawawezesha vijana kushiriki kiuchumi katika
ulimwengu wa digitali na kuabiliana na ushindani wa kimasoko.Hata hivyo
wanafunzi wa huo chake walioshiriki idadi ao ni 390 huku wanafunzi
wengine kutoka Kilimanjaro Film Institute (KFI).
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)