Pages

Mauzo ya tiketi za fastjet yazinduliwa Tanzania,Nauli za chini zaidi kuwahi kutokea kuna maana Watanzania wengi zaidi wanaweza kupaa

("fastjet" au Kampuni”)


Mauzo ya tiketi za fastjet yazinduliwa Tanzania

Nauli za chini zaidi kuwahi kutokea kuna maana Watanzania wengi zaidi wanaweza kupaa

13 Novemba 2012, Dar es Salaam - fastjet, Shirika la ndege la kwanza Afrika la nauli nafuu, leo limezindua mauzo ya tiketi zake nchini Tanzania, ikiwa ni maandalizi ya safari yake ya kwanza ya kibiashara mwishoni mwa mwezi huu.

Uzinduzi huo wa tiketi ni hatua muhimu katika juhudi za kampuni kuwezesha usafiri wa ndege kwa Watanzania wako wengi ambao awali walikuwa hawamudu gharama za safari za ndege. Huku nauli za anga zikiwa zinaanzia Tsh32, 000 (U$D20) kabla ya kodi za serikali, usafiri wa anga sasa unakuwa moja ya njia nafuu za watu kusafiri.

fastjet, ambayo imeinunua Fly540, imechagua Dar es Salaam kuwa kituo chake cha kwanza cha uendeshaji barani Afrika, huku safari za ndege zikiwa zimepangwa kuanza kuruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuanzia Novemba 29. Tiketi za Dar es Salaam – Kilimanjaro na Dar es Salaam – Mwanza zinaanza kuuzwa kuanzia leo. Safari zingine, za ndani na kanda ya Mashariki mwa Afrika, zitaanza baada ya wiki kadhaa.

Akizungumzia uzinduzi wa mauzo ya tiketi, Afisa Mtendaji Mkuu wa fastjet, Ed Winters alisema:

“Hiki ni kipindi cha kihistoria kwa safari za anga Tanzania, na hasa Afrika. Usafiri wa anga siyo tena himaya ya watu wachache Tanzania. fasyjet itafanya usafiri wa anga kuwa kitu ambacho Watanzania wengi wanakimudu tofauti na awali, na hivyo kutoa fursa nzuri zaidi kwa biashara, safari za likizo, na wanafamilia kutembeleana. Tunawashukuru wabia wetu Tanzania kwa ushirikiano wao mpaka leo hii, na tunamatumaini ya uhusiano mrefu na wenye manufaa kwa watanzania.”

Tiketi zinapatikana kupitia mawakala wa usafiri na dawati la mauzo, kituo cha mawasiliano na ofisi za fastjet yenyewe. Tovuti mpya ya fastjet, www.fastjet,com itazinduliwa wiki ijayo na kutoa taarifa za safari na nauli. Tovuti hiyo pia itaruhusu kununua tiketi kwa kutumia kadi za credit/debit pamoja na simu za mkononi.

Uzinduzi wa Chapa ya fastjet

Fastjet pia imezindua chapa yake mpya kabla ya kuanza kwa safari zake za kibiashara. Nembo ya  kampuni ni kasuku (kasuku wa kijivu wa Afrika) ambaye alichaguliwa kutokana na sifa zake za maarifa, urafiki na kuakisi kaulimbiu ya fastjet ambayo ni usafiri wa akili. Wiki hii pia itashuhudia uzinduzi wa mtandao wa kijamii wa fsaftjet kupitia Facebook na Twitter na hivyo kutoa ukumbi kwa wateja na wadau Kuwasiliana na kuchangia mawazo yao kuhusu kampuni kwa njia ya mtandao.

Richard Bodin, Afisa Biashara Mkuu wa fastjet anasema:

“Moja ya hulka kuu za fastjet ni uwazi. Tunataka kuziba pengo kati ya mlaji na shirika la ndege kwa kuhakikisha tunakuwa na mawasiliano ya pamoja kila inapowezekana na kusikiliza mahitaji na vipaumbele vya wateja. Mitandao ya kijamii ni njia bora ya kufanikisha hili – kumbi kama Facebook na Twitter hutuwezesha kuwasiliana moja kwa moja na wateja na kutusaidia sisi kuelewa vizuri zaidi na kuiwezesha fastjet kwenda sambamba na mahitaji na mapendeleo ya wadau wetu.

Shirika lina ndege tatu za kisasa aina ya Airbus A319. Ndege zote tatu zimo kwenye mchakato wa kupakwa rangi na nembo za fastjet kabla ya kuletwa Tanzania tayari kwa uzinduzi wa safari za kibiashara baadae mwezi huu.


MWISHO

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:

africapractice Tanzania  Tel: +255 (0)222 668 389

Teweli Teweli

Meg Muigai


Citigate Dewe Rogerson, London Tel:+44 (0) 20 7638 9571

Angharad Couch

Eleni Menikou



TAARIFA KWA WAHARIRI

Kuhusu fastjet Plc

fastjet Plc ni kampuni mama ya Shirika la Ndege la Afrika Fly540, ambalo hujiendesha kutoka vituo vinne Kenya, Tanzania, Ghana na Angola. Kwa sasa Fly540 ina ndege 10 zenye kuhudumia kama njia 25 za ndani na kanda, ikibeba takriban abiria 750,000 kwa mwaka, huku ikiwa na msisitizo mkubwa kwenye usalama, ulinzi na kuaminika.

Baada ya mashauriano na mwanzilishi wa easyjet, Sir Stelios Haji-Ioannou, kampuni ya easyGroup ililenga kubaini uwezekano wa kuwa na shirika la ndege la nauli nafuu Afrika, kama ilivyo Ulaya, na hivi sasa tunajiandaa kuzindua fastjet, shirika la kwanza la ndege Afrika la nauli nafuu, likiwa na ndege za kisasa kwa kutumia leseni na njia za Fly540. Safari za kwanza kwa kutumia chapa ya fastjet zinatarajiwa kuanza mwishoni mwa Novemba, na hivyo kuja na aina mpya kabisa ya safari za anga kwenye soko la Afrika.


fastjet Plc imeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la London (LSE). Kwa maelezo zaidi, tembelea www.fastjet.com

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)