SHIRIKA LA KAZI DUNIANI ILO LAWAJENGEA UWEZO WA VIJANA MKOANI ARUSHA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SHIRIKA LA KAZI DUNIANI ILO LAWAJENGEA UWEZO WA VIJANA MKOANI ARUSHA

Vijana  kutoka vyuo mbali mbali mkoani Arusha wameshiriki katika semina ya biashara iliyotolewa na shirika la wafanyakazi duniani (ILO) ikiwa ni njia mojawapo ya kuwajengea vijana uwezo  wa kujitegemea kiuchumi nje ya ajira.

Semina hiyo inalenga kutoa elimu na hamasa kwa vijana juu ya namna ya kuingia katika soko la biashara na kunufaika na fursa zilizoko katika soko hilo zitakazowawezesha kujikomboa kiuchumi na kuachana na utegemezi hasa wakutegemea kuajiriwa.

Billy Mushi ni Mjasiriamali ambaye ni mtoa mada anaeleza kuwa mafunzo hayo yamesaidia kuingiza watu wapya kwenye biashara hususani watu wa ngazi mbali mbali kutoka vyuoni,mashirika na benki na kuongeza kuwa vijana wanapaswa kujua kwamba wananaweza kufanikiwa endapo watatumia mbinu za kijasiriamali.

Tayari wameshatoa elimu hiyo kwa watu 1200 ambapo wanatoa mafunzo hayo si tu wale wenye uwezo wa kufundisha tu bali ni watu wenye uzoefu na waliobobea katika soko la biashara hivyo wanafunisha njia walizopitia ili kutoa hamasa kwa wengine kuthubutu kutumia fursa za kibiashara zilizoko kwenye maeneo yao ili waweze kufanikiwa kiuchumi,kimaisha na kutimiza ndoto zao.

Hata hivyo ametoa wito kwa vijana kushiriki katika semina,warsha mbali mbali na mafunzo  ya ujasiriamali ili kujijengea uwezo,maarifa na mbinu za kufanikiwa kiuchumi ili kuondokana na umasikini,utegemezi na tatizo sugu la ukosefu wa ajira linalowakabili vijana wengi nchini.

Joseph Mayagila ni Mkurugenzi wa Mafunzo katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha (AJTC) kilichoshiriki katika mafunzo hayo anasema kuwa mafunzo hayo hayawaandaa wanafunzi kutegemea mshahara tu bali yaawaandaa kufanikiwa kiuchumi aidi ya hapo ili mwanafunzi anapohitimu chuo aweze kujimudu kiuchumi mbali na kutegemea ajira peke yake.

Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa mafunzo hayo yatawawezesha vijana kushiriki kiuchumi katika ulimwengu wa digitali na kuabiliana na ushindani wa kimasoko.Hata hivyo wanafunzi wa huo chake walioshiriki idadi ao ni 390 huku wanafunzi wengine kutoka Kilimanjaro Film Institute (KFI).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages