Mkurugenzi wa Shirika la kazi nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo
akitoa hotuba yake siku ya kufunga maonyesho ya wajasiria mali MOWE 2012
yaliyokuwa yakifanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam.
Balozi wa Malawi nchini Tanzania Bi. Flossie Gomile Chidyaonga akitoa hotuba yake kwa wajasiria mali wa MOWE 2012.
Msichana Mjasiriamali akipokea cheti cha ushiriki wa MOWE 2012 toka kwa
Balozi wa Malawi Bi. Flossie Gomile Chidyaonga (kushoto). Katikati ni
Mwenyekiti wa Taasisi ya MOWE Bi. Elihaika Mrema.
Mkurugenzi wa ILO nchini Bw. Alexio Musindo (kulia) na Bi. Teddy Rucho
wakipokea cheti cha ushiriki toka kwa balozi wa Malawi katika sherehe za
ufungaji wa maonyesho ya wajasiriamali MOWE 2012.
Balozi wa Malawi Tanzania Bi. Flossie Gomile Chidyaonga (kushoto),
Mkurugenzi wa ILO nchini Bw. Alexio Musindo sambamba na Mwenyekiti wa
MOWE Bi. Elihaika Mrema (katikati) wakiangalia bidhaa zitokanazo na Mti
wa Mbuyu wakati wa sherehe za ufungaji wa maonyesho ya Wanawake
Wajasiriamali MOWE 2012 yaliyomalizika hivi karibuni katika viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar.
Balozi akitembea banda la ILO katika maonyesho ya MOWE 2012.
Balozi wa Malawi akipata maelezo toka kwa team ya ILO walioandaa maonyesho ya MOWE kwa kushirikiana na Taasisi ya WAMA.
Balozi wa Malawi na Mkurugenzi wa ILO nchini wakinunua mifuko maalumu ya
kuhifazia Laptops na iPad iliyotengenezwa kwa ubunifu mkubwa kwa
kutumia malighafi ya Tanzania Kitenge toka kwa Mwanamke Mjasiria mali wa
MOWE 2012 katika maonyesho hayo.
Bwana Pius Mikongoti wa GS1 akitoa Mada kuhusu Barcode kwa washiriki wa MOWE 2012.
Picha ya Pamoja Kamati ya MOWE na wageni rasmi siku ya kufunga maenyesho ya MOWE 2012.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)