Mtaalam na mshauri aliye
kwenye jopo la majadiliano kwa manufaa ya wote ( Smart Partnership)
Prof. Lucian Msambichaka akiongea na wahariri wa vyombo vya habari leo
jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa mkutano wa kimataifa wa
majadiliano kwa manufaa ya wote (Smart Partnership) kwa watanzania.
Mkutano huo utafanyika nchini mwezi mei 2013.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Ushindani la Biashara Tanzania (TNBC) Bw. Samson
Chemponda akitoa ufafanuzi kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusu
umuhimu wa mkutano wa majadiliano kwa manufaa ya wote (Smart
Partnership) na namna utakavyowawezesha watanzania kubadilishana uzoefu
kutoka kwa wataalam kutoka nchi nyingine kuhusu matumizi ya teknolojia
kuondoa umaskini kwa kutumia rasilimali zilizopo kwenye maeneo yao.
Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye semina kuhusu majadiliano kwa manufaa ya wote ( Smart Partnership) na nafasi ya vyombo vya habari katika kukuza
na kuimarisha uchumi na kuongeza uelewa miongoni mwa wananchi kuhusu
nafasi na fursa walizonazo katika kukuza uchumi nchini ikiwa ni sehemu
ya maandalizi ya mkutano wa kimataifa wa majadiliano ya pamoja
utakaofanyika nchini mwezi Mei 2013.
Meneja
Mradi wa Majadiliano kwa manufaa ya wote (Smart Partnership) Bi.
Rosemary Jairo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu namna
ambavyo wadau takribani 800 kutoka mataifa mbalimbali watakutana nchini
Tanzania kujadili kwa pamoja changamoto za kimaendeleo, kiteknolojia na
namna wananchi watanufaika kutokana na kutengeneza mtandao wa kutafuta
suluhisho la matatizo ya kiuchumi kutoka pande zilizofanikiwa. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)