Na Mohammed Mhina, Zanzibar
Kampuni ya Sauti za Busara
Zanzibar imesema kuwa haitaachana na Mwimbaji Mkongwe wa Muziki wa
Taarabu hapa nchini Bi. Fatuma Bint Mbaraska maarufu kama Bi Kidude hata
baada ya kutangaza kutaka kuachana naye. Katika taarifa yake kwa vyombo
vya Habari, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo inayoendesha Tamasha la kila
mwaka la Sauti za Busara visiwani Zanzibar Bw. Yusuf Mahmoud, imesema
kuwa kamwe kampuni hiyo haitamtupa Bi. Kidude.
“Wakati tunajuta kwamba baadhi ya
watu wanaamini vinginevyo, tunatarajia kutamka na kuthibitisha tena
kwamba tunatafuta na kuwafanyia wasanii kutoka Afrika Mashariki,
Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla, itaendelea kumsaidia Bi. Kidude
maisha yake yote”. Imesema sehemu ya taarifa hiyo. Hata hivyo taarifa hiyo
imeongeza kuwa Busara Promotion iko tayari kuzikabidhi fedha za Bi
Kidude kwake mwenyewe ama kwa mtu ambaye atatajwa na Bi. Kidude ili
mradi kuwa makabidhiano hayo yatafanyika kisheria yakiwahusisha
mashahidi tena wakiwemo mwanasheria, mwakilishi kutoka Serekalini na mbele ya Waandishi wa Habari ili kuepuka utata.
Hivi karibuni, Sauti za Busara
iliitisha mkutano na waandishi wa habari Zanzibar ili kuelezea juu ya
suala la muimbaji huyo hodari wa nyimbo za utamaduni Bi Kidude ambapo
ilitolewa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za mwimbaji huyo
zilizokuwa zikihifadhiwa na Sauti za Buisara. Mkutano huo uliohudhuliwa na
Waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari, uliitishwa kufuatia taarifa
za kudhulumiwa kwa fedha kwa Bi Kidude malalamiko ambayo yalikosa
kujulikana chanzo chake.
Hata hivyo katika mkutano huo
ilibainika kuwa kuna watu walionyuma ya pazia yaani mgongoni mwa Bi
Kidude ambao wanamhitaji kwa lengo ls kumtsgfunis frdhs zake kwa
kujifanya wasamalia wema. Waandishi waliitaka Sauti za
Busara kuendelea kumlea Bi Kidude na kuachana na maneno ya mitaani
ambayo yakishikiwa bango hayatakuwa na tija kwa Bi. Kidude ama
wanaojifanya wasamalia wema.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)