Katibu
Mkuu kiongozi Dr. Abdullhamid Yahaya Mzee akionesha Ripoti kwa
Waandishi wa Habari hawapo pichani juu ya kuzama kwa Meli ya M.V Skagit
iliotokea tarehe 18/07/2012 mwakahuu.
PICHA NA MAKAME MSHENGA -MAELEZO ZANZIBAR
………………………………………………………………………………………..
Na Mohammed Mhina, Zanzibar
Tume ya rais ya Zanzibar ya
kuchunguza chanzo cha ajali ya meli ya Mv Skagit, leo imetoa ripoti yake
kwa waandishi wa habari na kubainisha baadhi ya karoro na kutoa
mapendekezo ya hatua za kuchukua kwa wale wote waliohusikakatika ajali
hiyo.
Akitoa taarifa ya tume kwa
waandishi wa habari mjini Zanzibar, katibu mkuu kiongozi waSMZ Bw.
Abdullahamid Yahaya Mzee, amesema tume imebaini kuwa taarifa za idadi ya
abiria waliopanda meli siku ya tukio ilikuwa ni potofu.
Amesema tume hiyo imebaini pamoja
na mambo mengine, kuwa meli hiyo ilikua na idadi ya abiria 447 wakiwemo
watanzania 429 na raia wa kigeni 18 tofauti na idadi iliyotolewa awali
na uongozi wa meli hiyo kuwa ilikuwa na abiria 295 wakiwemo wafanyakazi
kumi wa meli hiyo.
Aidha tume hiyo pia imebaini kuwa
meli hiyo ilisajiliwa kinyume cha sheria na hivyo kupendekeza msajili
wa meli hiyo Bw. Seif Juma, kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu.
Hata hivyo taarifa ya tume hiyo
imetoautia na taarifa zilizokuwa zikitolewa na jeshi la polisi kuhusiana
na idadi ya maiti zilizokuwa zikipatikana siku hadi siku.
Katika ripoti ya tume hiyo,
imesema kuwa watu 81 walipoteza maisha tofauti na taarifa zilizokuwa
zikitolewa na jeshi la polisi kuwa hadi kufikia tarehe 11/8/2011, idadi
ya watu waliopoteza maisha ilikuwa ni 143.
Maiti za watu 222 zilipatikana
katika maeneo mbalimbali ya mwambao mwa bahari kwa upande wa Zanzibar na
nyingine 21 zikapatikana mkoani Tanga.
Hata hivyo baada ya kuonekana kwa
kasoro hiyo, baadhi ya waandishi walikuwa na wasiwasi kuwa huenda tume
hiyo haikupata taarifa kutoka polisi na madaktari waliofanya uchunguzi
wa miili iya watu liyokuwa ikipatikana siku hadi siku tangu kutokea kwa
tukio hilo.
Tume hiyo iliyokuwa ikiongozwa na
jaji wa mahakama kuu Mh. Abdruhakim Ameir Issa, pia imetoa mapendekezo
kuwa watu watano akiwemo mmiliki wa meli hiyo Bw.said Abdahamani Juma na
nahodha Bw. Mussa Makame Mussa pamoja na meneja mkuu wa kampuni ya Sea
Gull inayomiliki meli ya Skagit Bw. Omari Mnkonje washitakiwe
mahakamani.
Wengine wanaotakiwa kushitakiwa ni nahodha wa meli hiyo Bw. Makame Mussa na mhandisi wa zamu wa meli hiyo.
Meli ya MV Skagit ilizama tarehe
17/7/2012 katika baharini karibu na kisiwa kidogo cha Chumbe na
kusababisha vifo na manusura wa abiria waliopanda katika meli hiyo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)