Rais Jakaya Kikwete amechaguliwa
na kushinda kwa kishindo uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM taifa kwa
kupata kura 2395.kati ya 2397 zilizopigwa hii leo. Kwa matokeo hayo Ndugu
Jakaya Kikwete ameitetea vyema nafasi yake hiyo hadi mwaka 2017. Huku kura za hapana zikiwa 2. Sawa na asilimia 99.92.
Aidha wagombea wa Nafasi ya
Makamu Mwenyekiti ambazo kwa upande wa Bara ilikuwa ikigombewa na Katibu Mkuu
wa zamani wa CCM, Philip Mangula na amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM
Bara kwa kura 2397, huku nafasi ya Makamu
Mwenyekiti Zanzibar ameshinda Raius wa Zanzibar, Dk.Ali Mohamed Shein kwa
kupata kura zote zilizopigwa 2397. Ushindi wa Shein na Mangula kushinda kwa
kura za Ndio kwa Asilimia 100.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)