RAIS KIKWETE AWAFARIJI PAROKO WALIOJERUHIWA KWA RISASI IRINGA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RAIS KIKWETE AWAFARIJI PAROKO WALIOJERUHIWA KWA RISASI IRINGA


Waziri  wa nchi ofisi ya  waziri mkuu sera na uratibu  wa bunge  Mhe.Wiliam Lukuvi akimfariji Paroko Angelo Burgeo (60) wa parokia ya Isimani Iringa aliyelazwa  Hospitali ya mkoa  wa Iringa baada ya  kujeruhiwa kwa risasi na majambazi
Waziri  wa nchi  ofisi ya  waziri mkuu Sera na uratibu  wa bunge ,Wiliam Lukuvi ambaye ni mbunge wa jimbo la Ismani akimfariji msaidizi  paroko  wa Parokia ya Isimani  Herman Myalla (36) wa Kanisa aliyelazwa  Hospitali ya mkoa  wa Iringa baada ya  kuvamiwa na majambazi juzi
Picha na Habari na  Francis Godwin.

 Rais  Jakaya Kikwete  amewafariji paroko Angelo Burgeo (60) na msaidizi wake Herman Myalla (36)  waliojeruhiwa na majambazi  huku akiziomba taasisi  za dini  kutoa ushirikiano kwa  jeshi la polisi ili kuimarisha  ulinzi katika maeneo yao kama njia ya  kukomesha matukio ya ujambazi yanayofanyika katika maeneo ya taasisi za  dini.


Rais  Kikwete alitoa wito  huo kupitia waziri  wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), William Lukuvi ambaye ni mbunge  wa  jimbo la Isimani mkoani Iringa ambako paroko huyo na mwenzake  walivamiwa ,alitoa wito  huo  leo katika hospitali ya mkoa wa Iringa alipokuwa akiwasilisha salamu za Rais Jakaya Kikwete na kutoa pole kwa Paroko Angelo Burgeo (60) na msaidizi wake Herman Myalla (36) wa Kanisa Katoliki Parokia ya Isimani, wilayani Iringa.

Novemba 15, mwaka huu mapadri hao ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa wakiendelea na matibabu, walivamia na kushambuliwa kwa silaha za moto, mapanga na nondo na majambazi. Watu watano wanaosikiliwa na polisi wakihusishwa na uhalifu huo katika tukio hilo ambalo mapadri hao mbali na kujeruhiwa vibaya waliibiwa zaidi ya sh Milioni 3.8. Akiwasilisha salamu za Rais, Lukuvi alisema ametumwa kutoa pole kwa wahanga hao, waumini na viongozi wa dhehebu hilo la dini kwa ujumla wake.

“Tupo pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu ambacho majambazi wamekuwa wakiwavamia viongozi wa dhehebu hili la dini wakiamini mmehifadhi fedha na mali nyingine nyingi ndani ya parokia zenu,” alisema.

Alisema tukio la mapadri hao kuvamiwa na kujeruhiwa mkoani Iringa limekuja miezi michache baada ya matukio kama hayo kutokea katika parokia za Migori na Pawaga mkoani Iringa.

“Serikali imefanya kazi ya kutoa mafunzo kwa mgambo wengi karibu katika kila kijiji, ni wajibu wa taasisi hizi za dini kuwatumia hao au vinginevyo ikubali kushirikiana na jeshi la Polisi kutoa mafunzo kwa walinzi wao,” alisema.
Akipokea salamu hizo, Padro Burgeo alisema majambazi hao walifanikiwa kuingia ndani ya parokia yake baada ya kutumia lango la nyuma na kufanikiwa kuwapiga chenga walinzi wao. Alisema katika tukio hilo ilikuwa afe lakini Mungu amesaidia kuyanusuru maisha yake baada ya kufikishwa mikononi mwa madaktari.

Kaimu wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dk Faustine Gwanchele alisema baada ya kumfanyia upasuaji na kutoa risasi tatu kwa Padri Burgeo hali yake inaendelea vizuri pamoja na kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages