ZIMEZUKA habari zenye utata ambazo hazijathibitishwa mkoani Iringa kuwa mtoto mmoja anayedaiwa kufa na kuzikwa kuonekana jana akidaiwa kuwekwa Msukule.
Tukio hilo limetokea eneo la Mwangata mjini Iringa na kupelekea polisi kufika kuwatawanya wananchi waliokusanyika eneo hilo na kuwasaka wale wanadaiwa kueneza uvumi huo. Hata hivyo hakuna mwananchi hata mmoja kati ya waliokuwepo eneo hilo ambaye amethibitisha kuona msukule huyo zaidi ya kila mmoja kusema amesikia.
Wananchi hao wameizunguka moja kati ya nyumba eneo hilo wakitaka kuichoma moto kwa madai kuwa ndani kuna msukule huyo.
Habari / Picha kwa hisani ya : FRANCIS GODWIN BLOG





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)