Pages

MWEKEZAJI MWENYE ASILI YA KISOMALI ADAIWA KUMJERUHI ALIYEKUA MFANYAKAZI WAKE WAKATI AKIDAI HAKI YAKE

Aliyekuwa mfanyakazi wa Hoteli ya Yamiyami iliyoko mtaa wa Ohio jijini Dar es salaam Bw.Adrian Francis akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya kunyanyaswa na kufukuzwa kazi pamoja na kutopewa haki zake za msingi kutoka kwa mwajiri wake ajulikane kwa jina Fariha Guriti ambaye ndiye mmiliki wa Hotel hiyo ambapo Bw.Adrian Francis katika harakati zake za kudai haki zake leo alijikuta anaambuli kipigo kutoka kwa  ndugu wa mliki wa Hotel hiyo aliejulika kwa jina Abdul mwenye uraia wa kisomali kwa upande wake mmiliki wa hotel hiyo alikataa kutoa ushirikikiano kutoka kwa waandishi wa habari na kuhatarisha uhai wa maisha yao kwa kutaka kuwagonga na gari ili apoteze ushaidi wa picha.
Ndugu wa mliki wa Hotel hiyo aliejulika kwa jina Abdul mwenye uraia wa Kisomali katika akiwa chini ya ulinzi baada ya kumjeruhi  Bw.Adrian Francis  aliyekuwa mfanyakazi wa hoteli hiyo
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wakiwa wamelizingira la mmiliki wa Hotel ya Yamiyami Bi: Fariha Guriti baada ya kuwatishia waandishi wa habari kuwagonga na gari
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wakiwa wamelizingira la mmiliki wa Hotel ya Yamiyami Bi. Fariha Guriti baada ya kuwatishia waandishi wa habari kuwagonga na gari.PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)