Mwandishi wa
Sibuka afariki dunia kuzikwa Alhamisi
NA Andrew
Chale
MWANDISHI wa Habari
wa kituo cha SIBUKA, aliekuwa akitangaza na kuandaa vipindi mbalimbali
kikiwemo cha Pepeta Afrika, Lulu Oscar amefariki dunia jana Jumanne nyumbani kwao Mbezi Kwa Yusufu.
Akizungumza na .. mtandao/gazeti mdogo wa marehemu, Ritha Oscar
alisema kuwa Lulu alipatwa na mauti hayo
majira ya usiku ambapo alizidiwa ghafla kufuatia kulalamikia kifua kumbana.
“Awali alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Masister ya Luguluni kule Mbezi, zaidi ya mara
tatu, jana aliruhusiw kurudi nyumbani
lakini baada ya kuendelea vizuri lakini jioni usuku alilalamikia kifua
kikimbana tulimuangaikia mpaka hatua ya
mwisho lakini ikashindikana na alipoteza maisha” alisema Ritha kwa masikitiko
makubwa.
Ritha alisema kuondoka kwa Lulu kwenye familia yao ni pigo
kubwa kwani alikuwa bado ni mdogo na alikuwa msaada mkubwa kwa ndugu na jamaa.
Aidha, alisema kuwa, kikao cha muda cha ndugu kilichokaa
wameafikiana kuzikwa siku ya Alhamisi katika Makaburio ya Kinondoni. “Mpaka
sasa taarifa za familia, ni kuwa mazishi yatakuwa siku ya Alhamisi pale mkaburi
ya Kinondoni na msafara utaanzia nyumbani Mbezi kwa Yusufu na kuelekea
Makaburini” alisema Ritha.
Marehemu alikuwa mwajiliwa wa televisheni ya SIBUKA (TV
SIBUKA) akiwa kama mtangazaji na mwandaaji wa vipindi ambapo pia alikuwa
akiandaa na kutangaza kipindi cha Pepeta Afrika, kilichojizola umaarufu mkubwa
mpaka anakufa kwake.
Katika historia yake, Lulu alihitimu elimu yake ya msingi alihitimu mwaka 1996 katika shule
ya Upanga na kwa elimu ya uandishi wa habari alisomea chuo cha Royal College of
Tanzania na baadae mwaka 2003, aliweza
kuhitimu kozi zake hiyo ya juu katiika Taasisi ya uandishi wa habari na
mawasiliano Institute of journalisim and mass communication.
Marehemu alikuwa hajaolewa wala hajaacha mtoto.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)