Mke wa balozi wa Ireland nchini Tanzania (wa kwanza kushoto), Sarah Colins akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika katika ubalozi wa Uswisi, kuhusu maonesho ya hisani yatakayonyika siku ya jumamosi jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya watu wanaoishi katika mazingira magumu .na kufunguliwa na mke wa Makamu wa Rais Bi. Asha Bilal siku ya jumamosi. Pamoja nae ni Mwenyekiti wa kundi hilo Juliana Parroni (Switzeland) na Keiko Okada (Japan).
Mwenyekiti wa kundi la wake wa mabalozi nchini (DSG) Juliana Parroni,(kulia) akizungumza na waandishi wa habari, juu ya maonyesho ya hisani yatakayo fanyika siku ya jumamosi na kufunguliwa na Mke wa makamu wa Rais, Bi Asha Bilal kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa watu wanaoishi katika mazingira magumu. Kutoka kushoto ni mke wa Balozi wa Namibia Aletha Aisaack, Sara Colins (Ireland) Keiko Okada (JAPAN) na Kaisa Alapartanen (Finland).
Mke wa Balozi wa Japani nchini Tanzania (wa kwanza kutoka kulia) Keiko Okada, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari juu ya Maonyesho ya hisani yatakayofanyika mwisho wa wiki ili kuchangisha fedha kwa ajili ya makundi ya watu wasiojiweza, pamoja nae kutoka kushoto ni Mke wa Balozi waIreland Sarah Colins na katikati ni Mwenyekiti wa umoja huo Bi. Juliana Paroni. Maonyesho hayo yatafunguliwa na Bi. Asha Bilal Mke wa makamu wa Rais.
======== ======= =======
Maonyesho ya Hisani 2012
Siku ya furaha kwa mafanikio ya Watanzania.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Asha Bilal, anatarajia kuwa Mgeni rasmi katika Maonyesho ya Hisani yaliyoandaliwa na kundi la wake wa Mabalozi nchini. (DSG)
Maonyesho hayo yatakayo fanyika Novemba 17, mwaka huu katika viwanja vya Shule ya Kimataifa ya Tanganyika, jijini Dar es Salaam, hufanyika kila Mwaka kwa ajili ya kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia jamii zenye mahitaji maalumu hasa wanawake, watoto na walemavu wanaoishi katika mazingira magumu ikiwa ni mala ya pili Mke wa Makamu wa Rais kuendesha uchangishaji huo.
Mwaka 2011, Umoja huo kupitia maonyesho ya hisani ulikusanya jumla ya Shilingi milioni 73, ambazo zilisambazwa kama ufadhili kwenye miradi 15 ya hisani na taasisi binafsi Tanzania Bara na Visiwani, michango hiyo hufikia shilingi milioni 15 kwa kila kundi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)