Waziri wa Maliasili na
Utalii Mh. Balozi Khamisi Kagasheki anatarajiwa kuzindua mkakati wa
utangazaji utalii wa kimataifa tarehe 15/11/2012 katika hoteli ya Serena
hapa jijini Dar es salaam.
Mkakati huo unaotarajiwa kuwa ndio
dira ya kuitangaza Tanzania kama eneo la utalii duniani umetengenezwa
na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kushirikiana na Shirikisho la vyama
vya Utalii Tanzania (TCT) linajumuisha wadau mbali mbali katika sekta
ya utalii hapa nchini.
Hafla hiyo itakayofanyika kuanzia
saa 12.30 jioni itahudhuriwa pia na Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mh.
Lazaro Nyalandu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi
Maimuna Tarishi, Naibu Katibu Mkuu Bibi Nuru Milao na viongozi wengine
kutoka Wizarani. Aidha viongozi wa Shirikisho la vyama vya utalii nchini
TCT na wadau wengine wa sekta ya utalii watahudhuria pia hafla hiyo.
Fine!! Lakini vipi kuhusu utalii wa ndani? Kuna hatua zipi zinatekelezwa kwa ajili ya utalii wa ndani?
ReplyDeleteKwanini kila wizara,au sekta,au shirika la kibinafsi au la kiserikali lisitenge wiki moja katika mwaka,iitwe "WIKI YA UTALII" ili wafanyakazi na watumishi wapate fursa hiyo?? LET US REASONING ABOUT THIS TOGETHER!!