Mjumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphery Polepole (aliyesimama) akitoa
ufafanuzi wa vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977 kwa wananchi wa Kata ya Mliiba, Wilaya ya Tarime mkoani Mara
wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume hiyo leo alhamisi Nov.22, 2012.
Wajumbe wengine wa Tume, wa kwanza kulia Nassor Mohammed, Maria Kashonda
na Riziki Ngwali.
Wananchi
wa kijiji cha Mangucha Kata ya Nyanungu Wilaya ya Tarime mkoani Mara
wakifuatilia mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya
uliotishwa na Tume ya Mabadlliko ya Katiba leo alhamisi Nov. 22, 2012
katika kijiji hicho.
………………………………………………………………..
Na Ismail Ngayonga
Tarime, Mara
MKAZI wa Kata ya Kata ya Mliiba
Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Marco Magubo (31) amependekeza ni vyema
Katiba Mpya ikataze vyama vya siasa vinavyoingia madarakani mara baada
ya kushinda uchaguzi wa Rais visipeperushe bendera yake na badala yake
kuweka bendera ya Taifa.
Akitoa maoni yake leo (Alhamisi
Nov. 22, 2012) kuhusu Katiba Mpya kwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba alisema kitendo cha kupeperusha bendera ya chama kilichoingia
madarakani kitaongeza chuki kwa wanachama wa Chama kingine cha siasa
kilichoshindwa uchaguzi.
Aidha Magubo alisema Rais
anayeingia madarakani anawakilisha maslahi ya wananchi wote na hivyo si
busara kwa Chama kilichoshida uchaguzi kupeperusha bendera ya Chama chao
kwani Kiongozi huyo haongozi wanachama wa chama chake pekee bali
wananchi wote katika taifa.
“Tazama Marekani ambao hivi majuzi
tu walifanya uchaguzi mkuu wa Rais, katika kampeni za vyama vyao
hatukuweza kuona bendera ya Republican wala Democracy ambavyo vyote
vilishiriki uchaguzi na badala yake tuliona wananchi wakipeperusha
bendera ya Taifa lao na hatukuona bendera ya Republican wala Democracy”
alisema
Alisema kwa kuwa Tanzania ni nchi
ya umoja, amani na mshikamano ni vyema Katiba Mpya ikewe kipengele cha
kukataza bendera za vyama vyao na badala ya wamwachie Kiongozi aliyopo
madarakani kutetea hoja za wananchi wote.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)