Meneja wa
Baraza la Habari kanda ya Zanzibar(MCT)Suleiman Seif Omar akifafanua
jambo kwa Waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu tamko la Tume ya
utangazaji Zanzibar kupiga marufuku kuripoti taarifa za UAMSHO zenye
kuashiria uvunjifu amani kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa MCT John
P.Mireny
………………………….
Na Maelezo Zanzibar
Vyombo vya habari nchini
vimeshauriwa kujiepusha kuandika habari za uchochezi zinazoweza
kuhamasisha chuki ndani ya jamaii na hatimaye kuvuruga amani na
utangamano wa nchi.
Ushauri huo umetolewa na Kaimu
Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanaznia (MCT) John Mireny alipokuwa
akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Baraza hilo Mlandege
Zanzibar kuhusiana na Tamko lililotolewa na Tume ya Utangazaji Zanzibar
la kupiga marufuku matangazo yote yanayohusiana na vurugu zinazohusishwa
na wafuasi wa Jumuiya ya UAMSHO Zanzibar.
Amesema pamoja na ukweli kwamba
Baraza la Habari linatambua na kutetea kwa nguvu zote uwepo wa uhuru wa
Vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza, Baraza linasisitiza kwamba
vyombo hivyo vinawajibu mkubwa wa kulinda amani na jamii kwa ujumla.
Amesema Tume haikukosea kupiga
marufuku taarifa za Jumuiya ya UAMSHO zinazoashiria fujo na uvunjifu wa
amani na kwamba hizo ni taarifa ambazo hazikubaliki kutolewa katika
vyombo vya habari.
Hata hivyo ameongeza kuwa taarifa
zinazohusu UAMSHO ambazo hazihusiani na fujo na uvunjifu wa Amani
zinaweza kutolewa na vyombo vya habari nchini ili kuipasha jamii habari
za Jumuiya hiyo.
Ametoa mfano wa habari za Jumuiya
ya UAMSHO ambazo zinaweza kuripotiwa kuwa ni pamoja na mwendelezo wa
Kesi inayohusu Viongozi waandamizi wa Jumuiya hiyo Uchimbaji wa Visima
habari za kimaendeleo uchumi na kadhalika .
Nae Meneja wa Baraza hilo Kanda
ya Zanzibar Suleiman Seif Omar aliwataka wandishi wa habari kuwa
wadadisi na wafatiliaji kwa baadhi ya taarifa zinazo tolewa na vyombo
vya dola na isishie kukaa kimya bila yakupata ufafanuzi .
Aidha alifahamisha kua
iwapo mwandishi hakua makini katika kuandika habari zake na kuandika
habari za utenganishaji jamii, atambue kua jamii hiyo itakua ni vigumu
kuirejesha katika maelewano jambo ambalo halifai kwa mwandishi kufanya hivyo.
“Neno moja linaweza kuleta maafa
kwa jamii kwa hivyo wandishi wanapaswa wawe makini katika kutekeleza
kazi zao kwani amani ikitoweka ni vigumu kuirejesha”alisema Suleimani
Seif .
Aliwakumbusha waandishi kua fani
ya uandishi wa habari inamaadili yake yanayopaswa kufuatwa katika
kuandika habari na iwapo hayakufuatwa na kutanguliza ushabiki ni hatari
na inaweza kusababisha mtafaruku ndani ya jamii.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)