Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Dkt Shukuru J. Kawambwa (Kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Mamlaka
ya Elimu Tanzania (TEA), Rosemary Lulabuka (Kushoto) alipokutana na
waandishi wa habari kuzungumzia matembezi ya hisani ya kuchangia
ujenzi wa hosteli za wasichana wa sekondari yanayotarajia kufanyika
tarehe 17/11/2012.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Rosemary Lulabuka akiongea na waandishi wa habari juu ya matembezi ya hisani
ambayo yanalenga kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa hosteli
za wasichana wa shule za sekondar za kata.matembezi yatafanyika
jumamosi tarehe 17 Novemba 2012. Kuanzia Mlimani city.
Mwanamuziki
Barnabas akiongea na waandishi wa habari juu ya ushiriki wake katika kampeni na jinsi
atakavyochangia katika kampeni ya ujenzi wa hosteli za wasichana.
Mabalozi
wa hisani wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa hosteli za wasichana wakiwa na Meneja wa mawasiliano
wa TEA, Sylvia Lupembe Gunze (wa pili kutoka kushoto) na Msanii Barnaba
katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano wa Waziri wa Elimu
na Mafunzo ya Ufundi , Mh. Dr. Shukuru Kawambwa na waandishi wa
habari.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)