Mgeni
Rasmi Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Dkt. Abdallah Kigoda akitoa
hotuba katika Maadhimisho ya 23 ya Siku ya Viwanda Afrika yaliyofanyika
jijini Dar es Salaam leo, ambapo amesema hakuna nchi hapa duniani ambayo
imepata maendeleo ya kudumu kwa wananchi wake bila kuendeleza viwanda,
kwa sababu viwanda vinatoa ajira na hivyo kupunguza umasikini wa kipato
kwa wananchi wanaozalisha bidhaa viwandani.
Akifungua
maadhimisho hayo Mh. Dkt. Kigoda amesema Tanzania tunaendelea
kujijengea msingi bora wa kuendeleza viwanda vyetu ambapo jumla ya
viwanda vyote nchini ikijumuisha na mitambo ya kufua umeme ni takriban
733. Mapema
Mh. Dkt. Kigoda pia alizindua rasmi Ripoti ya Hali ya Ushindani wa
Sekta ya Viwanda Nchini 2012 ambayo pamoja na mambo mengine imetoa
mapendekezo kwa maeneo yanayoonekana yanahitaji msukumo ili kuongeza
kasi ya uendelezaji viwanda.
Maudhui
ya Ripoti hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa
kushirikiana na UNIDO yanashabihiana kwa karibu sana na kauli mbiu ya ya
mwaka huu. Kauli mbiu ya ya mwaka huu ni “Kuongeza Kasi ya Maendeleo ya Viwanda kwa Ajili ya Kukuza Biashara Baina ya Nchi za Afrika”.
Mwenyekiti
wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) Bw. Felix Mosha
akizungumza machache kumkaribisha mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa
katika maadhimisho hayo.
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou
akizungumzia Siku ya Viwanda Afrika na kusema kuwa ilitengwa na Umoja wa
Mataifa mwaka 1989 kwa madhumuni ya kuzitaka nchi za Afrika pamoja na
Jumuiya ya Kimataifa kubaini na kutambua umuhimu wa viwanda na mchango
wake katika maendeleo ya Bara la Afrika. Amesema
Siku ya Viwanda Afrika kwa mwaka huu inaangazia umuhimu ambao biashara
baina ya mataifa ya Afrika inaweza kuchangia kupunguza umasikini,
kuongeza akiba ya chakula na lishe na kuwezesha maendeleo endelevu. Uchumi
wa Afrika mpaka sasa kwa kiasi kikubwa umekuwa ukitegeme kilimo kama
uti wa mgongo, lakini viwanda ndio njia pekee ya kuweza kufanya
mabadiliko yatayowezesha kunyanyua uchumi wa mataifa ya Afrika. Moja ya vigezo vikubwa vya kufanya mabadiliko ni madiliko hali ya mifumo kutoka kilimo kuelekea viwanda.
Mgeni Rasmi Mh. Dkt. Kigoda akikata utepe kuzindua rasmi Ripoti ya Hali
ya Ushindani wa Sekta ya Viwanda Nchini 2012 iliyoandaliwa na Wizara ya
Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Shirika la Umoja la Maendeleo
ya Viwanda UNIDO, akisaidiwa na Mwenyekiti wa CTI Bw. Felix Mosha,
akishudiwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt.
Alberic Kacou.
Imezinduliwa rasmi..!!
Pichani ni baadhia ya wadau waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya
Viwanda Afrika wakiwemo mawaziri, waheshimiwa mabalozi, waheshimiwa
wabunge, makatibu wa kuu wa wizara, wakuu wa mashirika na waheshimiwa
washirika wa maendeleo.
Mgeni
rasmi katika Maadhimisho ya 23 ya Siku ya Viwanda Afrika Mh. Dkt.
Kigoda katika picha ya pamoja na mawaziri wa serikali, makatibu wakuu wa
wizara, wakuu na viongozi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, wakurugenzi
na maafisa wa taasisi mbalimbali na wadu wengine mara baada ya
kukamilika uzinduzi wa ripoti na hotuba japokuwa kongamano bado
linaendelea katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)