Mjumbe wa Jumuiya ya nchi za visiwa
katika bahari ya hindi Raj Mohabeer (katikati) akizungumza katika
mkutano wao na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif
Hamad nyumbani kwake Mbweni. Kulia ni mjumbe wa Jumuiya hiyoCorine Paya.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na Ujumbe wa nchi za visiwa katika
bahari ya hindi huko nyumbani kwake Mbweni Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Maalim Seif Sharif Hamad akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa
jumuiya ya nchi za visiwa vya bahari ya hindi pamoja na baadhi ya
watendaji wa Ofisi ya yake.Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
--
Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema Zanzibar inapata
manufaa makubwa kutokana na ushirikiano wake na Jumuiya ya nchi za
visiwa katika bahari ya Hindi.
Amesema Serikali inafuatilialia taratibu za kikatiba ili kuweza kuwa mwanachama kamili wa Umoja huo.
“Iwapo tutakuwa
wanachama kamili, mashirikiano yatakuwa makubwa na imara zaidi na bila
shaka manufaa yataongezeka”, alisema Maalim Seif.
Maalim Seif alieleza
hayo wakati akizungumza na ujumbe wa Jumuiya ya nchi za visiwa katika
bahari ya hindi yenye makamo makuu yake nchi Mauritius. Mazungumzo hayo
yalifanyika nyumbani kwake Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Amesema Visiwa vya
Zanzibar vinakabiliwa na uhaba wa ardhi kutokana na ongezeko la Idadi ya
watu, na kwamba serikali ina mpango wa kuelekeza ujenzi wa nyumba za
ghorofa katika maeneo ya mjini ili kukabiliana na tatizo hilo la
upungufu wa ardhi.
Kwa upande wake mjumbe
wa umoja huo Bwana Raj Mohabeer amesema Zanzibar itaendelea kunufaika
na mashirikiano ya nchi za visiwa hata kama si mwanachama wa umoja huo.
Amesema umoja huo
umevutiwa na mazingira ya Zanzibar na kuelezea matumaini yake kuwa
Jumuiya hiyo itakuwa ikifanya mikutano yake hapa Zanzibar angalau mara
moja kwa mwaka.
Nchi hizo za visiwa
katika bahari ya Hindi zinashirikiana katika maeneo tofauti yakiwemo
kukabiliana na majanga, mabadiliko ya tabia nchi pamoja na uhifadhi wa
mazingira ya baharini.
Na
Hassan Hamad
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)