JOHN GININITA MAKAMU MWENYEKITI MISS UTALII TANZANIA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

JOHN GININITA MAKAMU MWENYEKITI MISS UTALII TANZANIA

Bodi ya Miss Tourism Tanzania Organisation,yenye dhima ya kikomo ya kuaandaa na kuendesha mashindano ya Miss Utalii Tanzania ,imemteua Ndugu John Guninita kuwa Makamu mwenyeketi ya bodi ya Mashindano ya Miss Utalii Tanzania. Uteuzi huo utakuwa ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 22-10-2012.

Akuthibitisha uteuzi huo, Gideon Chipungahelo, Rais wa Miss Utalii Tanzania, hatua hii ni moja ya utekelezaji mpango mkakati wa kuimalisha mashindano na uongozi wa mashindano haya.

Mabadiliko ya mfumo wa uongozi na uendeshaji wa mashindano ni pamoja na kuinalisha uongozi, na ni hatua madhubuti za ulifanya shindano la Miss Utalii Tanzania kuwa shindano bora na kubwa zaidi hapa nchini ,Afrika na nje ya bara la Afrika.

Uteuzi huu wa Ndugu Guninita ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkoa wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam ,ni kutokana na bodi kuzingatia busara,hekima na uzoefu mkubwa katika uongozi wa Jamii na jumuiya mbalilmbali za kutaifa na kimataifa.

Bodi inaamini kuwa uwepo wa Ndugu Guninita kama Makamu mwenyekuti katika bodi ya mashindano haya,sambamba na wajumbe wengine wateule wa bodi ,kutafungua ukurasa mpaya kwa mashindano haya, ambayo ni dira na mwelekeo wa dhati wa kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi za Afrika na Dunia kwa ujumla

Asante,
Gideon Chipungahelo
Miss Utalii Tanzania Alama ya urithi wa Taifa – Ewe Mtanzania Tembelea na tangaza Hifadhi za Taifa – Utalii ni Maisha , Utamdauni ni Uhai wa taifa

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages