Elimu ya Utowaji wa Maoni ya Katiba Mpya kwa Wananchi wa Zanzibar. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Elimu ya Utowaji wa Maoni ya Katiba Mpya kwa Wananchi wa Zanzibar.

  Mtoa mada Saleh Mohammed , wa Baraza la Katiba Zanzibar akitowa mada katika mkutano wa siku moja juu ya Zanzibar katika Mchakato wa kutowa maoni ya Katiba Mpya unaoendelea Tanzania nzima,Maoni ya Katiba wiki ijayo yataaza katika  Mkoa wa Mjini Magharibi , ili wananchi kupata nafasi kutowa maoni yao jinsi ya mfumo wa Katiba ya Jamuhuri ya  Muungano wa Tanzania.  
 Profesa Abdul Shariff,Mwenyekiti wa Baraza la Katiba Zanzibar , akitowa mada ju ya mchakato wa kuchangia maoni ya Katiba Mpya ya Tanzania, kuhusu mfumo wa Serekali mbili za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ,  wakati akitowa Elimu kwa Wananchi jinsi ya kuchangia Katiba ya Mpya ya Tanzania , Inayotarajiwa kuaza kutowa maoni yao Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi jumatatu wiki ijayo katika maeneo mbalimbali ya mjini wa Unguja.
  Viongozi wa meza kuu wakifuatilia michango ya Wananchi wakati wa kutowa elimu ya mchakato wa kutowa maoni ya Katiba Mpya Tanzania.uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani ukumbi wa salama.
 Wananchi wakisikiliza Mada zinazowasilisha katika mkutano wa siku moja wa kutoa elimu ya mchakato wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, mkutano huo umeandaliwa na Baraza la Katiba Zanzibar.iliofanyika katika ukumbi wa salama bwawani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages