Bi Arafa Issa Namaji (Pichani) mwenye umri wa miaka 39 mkazi wa kijiji cha Narung’ombe wilayani Ruangwa Mkoani Lindi anaomba msaada wa haraka utakaomuwezesha kupata matibabu ya uvimbe ulio katika paji la
uso uliotokana na maumivu makali ya kichwa baada ya kupata matibabu katika hospitali ya Ndanda na kuelekezwa kufika katika hospital ya Taifa ya Muhimbili(MNH) Kwa uchunguzi zaidi na matibabu.
Tatizo lilianza tangu mwezi february 2012,alianza kwa kuumwa na kichwa kwa maumivu makali sana na kipele kidogo kikatokea kwenye paji la uso,hivyo basi kadri kilipopungua maumivu ndipo kipele kiliendelea kuwa kikubwa hadi kuathiri macho na sehemu ya pua.
Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya Majirani na marafiki wa karibu walimshauri kwenda hospitali ya wilaya,alipofika Daktari alimpa rufaa ya kwenda hopsitali ya Ndanda,hata hivyo Ndanda pia wakampa rufaa kwenda hospitali ya rufaa muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
kutokana na hali hali hiyo ngumu aliyonayo Kutokana na kuwa katika hali duni na hana mtu yeyote wa kumsaidia Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa wameichangishana kupata kiasi cha nauli pamoja na hela kidogo ya kujikimu kwa sikumbili,lakini bado anahitaji msaada zaidi wa pesa kwa sababu atahitaji kuishi zaidi DSM Akiwa katika hospital ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi pamoja na matibabu yake.
Kwa alietayari kumsaidia anaweza kuwasiliana na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Lindi ambae pia ni mwakilishi wa Channel ten,Abdulaziz Ahmeid kwa namba za simu 0787176221 au 0756696048
Kutoa ni Moyo ili kumsaidia mama huyu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)