Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 15 kutoka kwa Robert Pascal Mkuu wa Kitengo cha Kilimo benki ya NMB, kama mchango wa benki hiyo kwa ajili ya kununulia madawati ya shule za msingi katika mkoa huo, Ikiwa ni mchango wa benki hiyo katika maendeleo ya elimu Mkoani Katavi, ambao umezinduliwa rasmi na Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda, na kuhudhuriwa na wananchi wengi wa mkoa huo. Mbali na fedha hizo benki ya NMB pia imetoa kiasi cha shilingi milioni 15 zingine na vifaa vya michezo ikiwemo mipira na jezi kwa ajili ya timu za mpira wa miguu za mkoa wa Rukwa na Katavi kwa ajili ya kufanikisha mchezo wa mpira wa miguu kati ya timu hizo wakati wa uzinduzi katika mkoa huo , pamoja na maandalizi mengine ya shughuli za uzinduzi, jumla ya fedha iliyotolewa na Benki ya NMB ni shilingi milioni 30 za Kitanzania.
Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal akizungumza na wafanyakazi wa benki ya NMB wakati alipotembelea banda la benki hiyo katika maonyesho yaliyofanyika wakati wa uzinduzi wa mkoa mpya wa Katavi mjini Mpanda.
Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal (kushoto) akiteta jambo na Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda, wakati wa kutathmini mrejesho wa kongamano la Uwekezaji katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika uliofanyika Oktoba 17 mwaka jana mjini Mpanda.
Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe akikaribisha wageni mbalimbali waliofika kwa ajili ya uzinduzi wa Kongamano hilo na Mkoa wa Katavi lililofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Maji Mjini Mpanda hivi karibuni.
-





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)