Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenekiti wa Baraza la Mapinduzi Mwinyihaji Makame Mwadini atembelea Maonyesho ya vitu mbalimbali vilivyotengenezwa na wazee wa Sebleni Zanzibar katika Maadhimisho ya siku ya wazee duniani - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenekiti wa Baraza la Mapinduzi Mwinyihaji Makame Mwadini atembelea Maonyesho ya vitu mbalimbali vilivyotengenezwa na wazee wa Sebleni Zanzibar katika Maadhimisho ya siku ya wazee duniani

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenekiti wa Baraza la Mapinduzi Mwinyihaji Makame Mwadini akisalimiana na mmoja ya Wazee bi Raya Abdallah Masaku baada ya kuangalia vitu ambavyo wazee hao wa Sebleni wanavitengeneza katika maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani
   Baadhi ya wazee ambao wanatunzwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika nyumba za Sebleni Amani mjini Zanzibar wakiwa wanasikiliza hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani)katika maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo octoba 1
Baadhi ya wazee ambao wanatunzwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika nyumba za Sebleni Amani mjini Zanzibar wakiwa wanasikiliza hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani)katika maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo octoba 1.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
---
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
 
Serikali ya Mapinduzi Zanzíbar imesema kuwa imepanga sera na mikakati ya kuwaenzi na kuwathamini wazee wote pamojana kuwawekea jitihada za kuhakikisha wanapata mustakbali mwema wa maisha yao .
 
Hayo yameelezwa jana huko Nyumba za Wazee Sebleni wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame kwa niaba ya Rais wa Zanzíbar na Mwenykiti wa Baraza la Mapinduzi .
 
Alisema kuwa serikali ipo katika mchakato wa kuandaa sera ya hifadhi ya jamii ambayo itazungumzia maslahi ya makundi yote katika jamii ikiwa ni pamoja na wazee
Aidha alisema kuwa wazee wanahitaji kuenziwa na kudhaminiwa kutokana na kuishiwa nguvu za mwili na kukosa uwezo wa kufanya kazi.

Aidha akifahamisha kuwa jitihada za Serikali zinatarajia kufikia hatua nzuri za kuweza kuwapunguzia umaskini kwa kuwawezesha wazee wote waliyofanya kazi katika serikali na wale ambao walifanyakazi zao binafsi kuweza kuwakomboa na umasikini uliokithiri na kufikia lengo kuu la millenium.
 
Dk Mwinyihaji alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzíbar imeeandaa mambo maalum kwa ajili ya wazeee ikiwemo pencheni nzuri kuimarishiwa huduma za afya ndani ya makaazi yao kwa wale wazee wanaishi makaoni na kuweza kuimarisha ustawi wa wazee kwa kuwawezesha kuwapa mafunzo mbali mbali ili kuwajengea uwezo wazee hao.
 
Nae Waziri wa Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Vijana na Watoto Zainab Mohammed alisema kuwa anaipongeza serikali kwa kuweza kuitambua siku hii athimu ya wazee ya kuweza kuwawekeawazee misingi imara ya kuwatunza kuwaenzi na kuwathamini .
 
Aidha alisema kuwa leo ni siku ya faraja Kubwa kwa kupata fursa ya kusherehekea siku hii adhimu ya wazee duniani .“Kwani mzee ameitwa mzee kwa kuishiwa na nguvu za kujihudumia kwa kiasi kikubwa amesema’’ Waziri Zainaab

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages