Imeelezwa kuwa TV zote zikiwemo
zile zenye migongo, matumbo na viuno virefu zote zina uwezo sawa wa
kupokea matangazo ya digitali na Watanzania waepuke uvumi wa watu
wachache wanaodai kuwa TV za zamani hazitapokea zitafutwa mara Tanzania
itakapoingia kwenye mfumo wa Digitali.
\
Wito huo umetolewa na Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano hapa nchini TCRA ambaye pia na
Mratibu wa Ofisi za Kanda Bw. Victor Nkya, wakati wa mkutano wa
Wataalamu wa Mawasiliano ya Habadi kwa njia ya digitali kutoka nchi za
SADC unaojadili umuhimu wa mfumo wa Digitali.
Bw. Nkya amesema kuwa wananchi
hawana haja ya kuwa na hofu juu ya TV walizonazo zikiwemo zenye matumdo
na migongo mikubwa kuwa hazitaweza kupokea matangazo ya televishen
katika mfumo mpya wa digitali.
Amesema kutokana na watu wengi
kutumia televishen za Analojia, ni lazima kila mmoja wetu awe na
kingamuzi na kazi ya Mamlaka ya mawasiliano ni kuwajengea wananchi
matumaini na kuepuka kudanganywa.
Kwa siku za hivi karibuni baada
ya Tanzania kuridhia mabadiliko ya mfumo wa Digitali, wananchi wamekubwa
na wasiwasi wakidhani kuwa huo ndio mwisho wa tv za zamani.
Awali akifungua Mkutano huo wa
siku tatu hapa mjini Zanzibar, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano
Zanzibar Mh. Rashid Suleiman, amewataka wananchi kukabiliana na
changamoto mbalimbali zitakazojitokeza wakati wa mabadiliko ya kutoka
katika mfumo wa analojia na kuingia katika digitali.
Amesema ni vema wananchi wakahama
mapema kutoka katika mfumo huo wa zamani ili kuepuka usumbufu wakati
yatakapotokea mabadiliko hayo kwani hakutakuwa na muda wa nyongeza kama
Watanzania walivyozoea.
Na kuna umuhimu wa wananchi pia
kusikiliza maelekezo ya wataalamu badala ya kusikiliza propaganda za
watu wasio na ujuzi juu ya teknolojia hiyo.
”Watanzania hawana haja ya
kuogopa na badala yake wajiandae kujipatia vingamuzi na kinyume cha
hivyo watashindwa kupata matangazo ya televishen kama wanavyotarajia.”
Alisema Waziri.
Amesema kila mabadiliko yana
hasara na faida zake, lakini kwa mabadiliko ya kutoka katika mfumo wa
analojia kwenda digitali, kuna faida kubwa na moja ya faida hizo ni
kuwawezesha watu wote kupokea matangaza sawa na yenye ubora unaofanana
na kwa wakati muafaka.Mkutano huo wa siku tatu unazishirikisha nchi zote
za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC ikiwemo Angola,
Afrika ya Kusini, Malawi, Namibia, Botswana, Swazlland, Lesotho,
Msumbiji na wenyeji Tasnzania.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)