Spika Wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh Anna Makinda.
Mhe. Anna S. Makinda (Mb) Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania anatarajia kuongoza Ujumbe wa Waheshimiwa Wabunge Wanne
Kushiriki Mkutano na Jumuiya ya Umoja wa Mabunge Duniani Inter -
parliamentary Union (IPU) utakaofanyika mjini Qubec nchini Canada
kuanzia tarehe 21 – 26 Oktoba 2012 ikiwa ni sehemu ya kuimarisha
diplomasia ya kibunge(Parliamentary Diplomacy).
Ujumbe huo wa Waheshimiwa Wabunge utakaoshiriki Mkutano huo kutoka Tanzania ni pamoja na:
Mhe. Hamad Rashid Mohamed (Mb)
Mhe. Susan L. Lyimo, (Mb)
Mhe. David Kafulila (Mb) na
Mhe. Dkt. Pudenciana kikwembe (Mb)
Agenda kubwa ya Mkutano huu ni kulenga kuendeleza Mahusiano ya Mabunge
Duniani katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii sanjari na
demokrasi ya kweli inayohusu mjadala uliopewa jina la Uraia, Utambulisho
na Lugha, na Mtambuka wa Kuutamaduni katika Dunia ya Utandawazi
(Citizenship, identify and linguistic and culture diversity in a
globalized world).
Pamoja na mjadala kuhusu mada hii, Wabunge katika Jumuiya hiyo
watajigawa katika kamati mbalimbali kujadili masuala mbalimbali ya
kibunge ambayo yamepewa mada zifuatazo:-
Enforcing the Responsibility to protect the Role of Parliament in Safeguarding civilians lives
Fair Trade and innovative financing mechanism for sustainable development
The use of media including social Media to enhance citizen engagement and democracy
Aidha taarifa ya Jumuiya ya Umoja wa Mabunge Dunia (IPU) kuhusu
mahusiano yake na umoja wa Mataifa itatolewa kwa washiriki wa Mkutano
huo ikifuatiwa na Mijadala mingineyo saba amabayo itakuwa na maada
zifuatazo:
Mahusiano ya Nchi na nafasi ya diplomasia ya Kibunge (Multilateralism and the role of Parliamentary Diplomacy)
Mahitaji Makubwa ya Mafuta: Nini Matarajio ya Usalama wa Nishati (Peak Oil: What prospects for energy security
Ujengaji wa amani baada ya Migogoro (Building Peace after Conflict)
kujenga fursa za Vijana katika uchumi wa kitandawazi (Creating Opportunities for youth in today’s global economy)
Kinga za Kibunge: ni kwa manufaa au Mzigo? (Parliamentary immunity: benefit or burden?)
Bunge na sheria za siasa, (Informal Panel: Parliamentary and political law)
Warsha kuhusu nyenzo mpya za kuwezesha kupunguza matumizi ya nguvu za
nuclear (Workshop on new tools to promote Nuclear disarmament).
Pamoja na mijadala hiyo ujumbe wa Tanzania Utakutana na Katibu Mkuu wa
Jumuiya hiyo Ndg.Anders B. Johnsson na kufanya mazungumzo ya pamoja
kufuatia Tanzania kupewa heshima ya kuwa mwenyeji wa kuandaa Semina ya
Wabunge wanawake wa Jumuiya hiyo kutoka nchi za Afrika ya mashariki,
Afrika ya kati na kusini mwa Afrika.
Semina hiyo itakayofanyika Tanzania itakuwa na mada kuhusu Mwitikio na
nmana ya kuzuia ukatili dhidi ya Wanawake: kutoka Utungaji wa Sheria
Husika hadi kufika utekelezaji wake (Preventing and Responding to
violence against Women: From legislation to effective enforcement) na
itafanyika Dar – es- Salaam tarehe 5 – 7 Desemba 2012 ambapo wajumbe
zaidi ya 100 kutoka nchi 15 za SADC na Africa Mashariki watashiriki .
Sambamba na Mkutano huo, Makatibu wa Mabunge kutoka nchi wanachama
watafanya vikao vitakavyo jadili masuala mbalimbali ya kiutendaji ambapo
katibu wa Bunge Dr. Thomas D. Kashililah atawakilishwa na Ndugu Kileo
Nyambele Mkurugenizi wa Maktaba na Utafiti wa Bunge.
Ujumbe wa Tanzania unatarajia kurejea nchini tarehe 28 Oktoba, 2012.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)