Mchungaji
Kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni Mh. Dkt. Getrude
Rwakatare akitoa Ujumbe kwa Watanzania waliohudhiria Ibada Maalum ya
Kuliombea Taifa ambapo ametaka watu kutobaguana kwa misingi ya Dini,
Ukabila wala Siasa na kusema pamoja na Utawala bora pia tunahitaji
maombezi ili tuweze kufikia Malengo yaliyokusudiwa kulipeleka Taifa
linapotakiwa kufikia.
Dkt.
Rwakatare amesema nia kubwa ya kufanya Ibada hiyo ya Maombezi ni kutaka
kuweka usawa kutokana na siku za hivi karibuni kuibuka kwa Matamko
mbalimbali kutoka kwa watu tofauti wakiwemo viongozi wa Kitaifa, Kidini
na wa baadhi ya Makundi yanayohitilafiana na kusema tukiomba kwa jina la
Mungu kila kitu kitakwenda kama tulivyomuomba ili Tanzania iendelee
kuwa nchi ya Amani na Utulivu kama ilivyokuwa miaka yote ambayo ni
kimbilio la watu wa Mataifa mbalimbali kwa sababu Watanzania hawajui
kuchukiana na wamekuwa watu wa kushikamana kwa miaka yote.
Picha Juu na Chini ni Waumini waliohudhiria Ibada Maalum ya kuliombea
Taifa wakinyanyua bendera juu kuimba na kuabudu kwa furaha bila
kuonyesha tofauti ya matabaka.
Msanii
wa Kimataifa wa muziki wa nyimbo za Injili wa Tanzania Rose Muhando
akiimba na kumtukuza Mungu sambamba na wachezaji wake wakati wa Ibada
hiyo maalum ya kuliombea Taifa letu liendelee kuwa na Amani, Upendo na
Utulivu.
Nimeonja Utamu wa Yesu Weeeeee........!!!
Mchungaji Kiongozi Dkt. Rwakatare akijumuika sambamba na waumini wakiabudu na kuimsifu Mungu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)