Mstahiki meya wa halmashauri ya wilaya ya Ilala Mhe. Jerry Silaa
akijaribu kufafanua jambo mbele ya waandishi (hawapo pichani) juu ya
mapato ya Halmashauri yake kwa mwaka wa fedha 2012-13
Mstahiki meya wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Jerry Silaa
akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Anatouglo Mnazi Mmoja kuhusu
mapato ya Halmashauri ya Wilaya hiyo na hali halisi ilivyo katika bajeti.
---
Baraza la Halmashauri
ya Wilaya ya Ilala, kupitia meya wake, Mhe. Jerry Silaa jumatatu ya Oktoba 1,
2012 amekutana na waandishi wa habari pamoja na wafanyabiashara katika ukumbi wa
Amaoutoglu kuzungumzia kwa ufupi juu ya utendaji wa shughuli za manispaa ya
ilala kwa mwaka wa fedha 2011/2012.
Manispaa ya Ilala kwa
mwaka uliopita imefanya jitahada kubwa juu ya ukusanyaji wa mapato huku ikipitia
changamoto mbalimbali ambazo baadhi zimepatiwa ufumbuzi. Kwa ujumla, ukusanyaji
wa mapato uliokusudiwa umepanda kutoka 88% kwa mwaka wa fedha 2010/2011 mpaka
Shilingi 17.1 bilioni zilizokusanywa mwaka huu kiasi ambacho ni sawa na 99% ya
mafanikio ya malengo.
Ongezeko hilo limetokana na kugundua vyanzo vingi vya
mapato kwa 102% ambavyo ni Shilingi 2.25 bilioni kutoka katika mabango ya
matangazo yaliyopo barabarani. Kiwango hicho kimeongezeka kutoka shilingi 1.47
bilioni ya mwaka jana mpaka shilini 2.25 bilioni mwka
huu.
“Leo tumewalika walipa
kodi wakubwa katika manispaa ya Ilala ambao mchango wao katika uchumi wetu
umekuwa mkubwa sana . Sababu kubwa ikiwa ni kuwapa walipa kodi taarifa fupi na
kuwashukuru kwa mchango wao katika maendeleo ya manispaa yetu. ”Alisema Mstahiki
Meya Mhe. Jerry Silaa.
Kitengo kingine
kilichoonyesha mafanikio ni kile kinachotoa leseni za ujenzi ambacho kimechangia
ongezeko la 205% ambalo ni shilingi 307 milioni kutoka shilingi 154 milioni ya
mwaka wa jana.
Kutoka shilingi 2.14
bilioni za makusanyo ya mapato kutoka kwenye kodi ya thamani, lengo hili
lilishuka kwa kiasi kikubwa mpaka 54% kutoka kwa malengo yaliyowekwa
ukilinganisha na 74% kwa mwaka jana. Sehemu iliyofanya vibaya kabisa kwa mwaka
huu katika ukusanyaji wa mapato ni mapato kutoka leseni za biashara ambayo
0%.
Kutokana na kutofikia
malengo, kazi za maendeleo zilizopangwa na halmashauri kwa ajili ya maendeleo
zimekuwa na changamoto kubwa. Mwaka wa fedha wa 2012/13 umeshapangwa na
tunatarajia kuomba msaada si tu kwa Wafanyabiashara na wakazi wa Halmashauri wa
manispaa ya Ilala kwa kiasi kikubwa ila pia tunaitegemea serikali kuu katika
hili. Asilimia 49 tu ya bajeti ndiyo imepatikana tayari kwa mataumizi ya miradi
ya maendeleo ya manispaa.
“Manispaa ya Ilala ipo katika moyo wa jiji la Dar es salaam, na nchi kwa ujumla kutokana na ofisi nyingi za serikali, ofisi nyingi za makampuni pamoja na ofisi za kibalozi zipo katika Halmashauri yetu, kutokana na hilo, ninaomba Serikali kuangalia juu ya ufanikishaji wa mapendekezo wa bajeti yetu kwa mwaka wa fedha 2012/13 kwa asilimia 100 ili kuweza kufanikisha mahitaji muhimu ya maendeleo ya Halmashauri na kuwezesha ufanyaji wa shughuli mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri yetu” alimalizia meya.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)