Lile tamasha kubwa kuliko yote
hapa nchini, maarufu kama Serengeti Fiesta ambalo limekuwa likizunguka
mikoa ya Tanzania bara na kufika takribani mikoa 11 sasa linaelekea
katika kilele chake katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam
siku ya jumamosi wiki hii ambapo msanii wa hiphop kutoka nchini
Marekani Leonard Roberts maarufu kama Rick Ross atatumbuiza katika
tamasha hilo.
Akizungumzia ujio wa msanii mkubwa
kama huyo katika mahijiano maalum jijini Dar es Salaam jana, meneja wa
bia ya Serengeti bw. Allan Chonjo amesema tamasha la Serengeti Fiesta
limekuwa likifanya vizuri sana katika mzunguko wake na kwamba watanzania
wamekuwa wakifurahia uwepo wa tamasha hilo kutokana na mafanikio
mbalimbali ambayo wamekuwa wakiyapata kila ilipofika msimu wa Serengeti
Fiesta “mwaka huu tutakuwa na Rick Ross na kwamba watanzania waendelee
kujenga imani na Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake ya
Serengeti Premium Lager, kwani kila kilele cha msimu wa tamasha hili
ndio mwanzo wa maandalizi ya msimu unaofuata”.
Rick Ross ambaye ni mmoja kati ya
wasanii wanaotamba sana katika miondoko ya kurap (hip hop) nchini
marekani, atawasili hapa nchini siku ya alhamisi tayari kabisa
kutumbuiza katika maadhimisho ya kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta
siku ya jumamosi mwishoni mwa wiki hii.
Msimu wa Serengeti fiesta ulianzia
katika mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Musoma, Shinyanga, Mwanza, Tabora,
Singida, Dodoma, Morogoro, Mbeya na Iringa ambapo wakazi wake walipata
burudani na ladha ileile ya bia ya Serengeti kabla ya kufikia mwisho wa
msimu wake wiki hii. Wasanii waliburudisha katika
tamasha la Serengeti Fiesta nyanda za juu kusini ni pamoja na Inspector
Haroun, Juma Nature, Roma Mkatoliki, Linah, Amini, Supa nyota Serengeti
fiesta 2012 na wengine.
Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es
Salaam na mikoa ya jirani wanatarijwa kumiminika katika viwanja vya
Leaders Club kushuhudia burudani mbalimbali zitakazotolewa na wasanii wa
hapa nchini, kabla ya kilele cha msimu wa ‘BHAAAS’ kumaliziwa na msanii
Rick Ross na kundi lake kwa kiingilo cha shilingi 20,000/= za
kitanzania kwa wale watakaonunua tiketi zao mapema na elfu 25,000/= kwa
wale watakaonunu tiketi getini.
Katika tamasha la Serengeti Fiesta
msimu wa uliopita uliokuwa ukijulikana kama ‘Haina Majotroo’ Kampuni ya
bia ya Serengeti iliwaleta wasanii maarufu ambapo msanii wa muziki wa
raga ‘Shaggy’ alitumbuiza katika uzinduzi wa msimu huo jijini Mwanza na
msanii nyota kutoka nchini Marekani Ludacris alihitimisha msimu wa kwa
kuwaburudisha wakazi wa jiji la Dar Es Salaam na majirani zake kama
kawaida katika viwanja vya Leaders Club.
Umaarufu wa tamasha Serengeti
Fiesta umekuwa ukitengeneza ajira mbalimbali za muda mfupi na kudumu, na
pia nyingine zikianzishwa kupitia Serengeti Fiesta katika maeneo yote
ambayo tamasha hilo lilipata kupita zikiwemo kuibuliwa kwa wasanii
chipukizi na baadaye kujitegemea kimuziki, kujengeka kwa majina ya
wasanii mbalimbali ambao hawakupata kufahamika zaidi kwa mashabiki wa
muziki pamoja na kuibuka kwa wasanii wa filamu kupitia tamasha hili la
Serengeti Fiesta,linalodhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia
bia ya Serengeti Premium Lager.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)