Meneja
Mauzo na Masoko wa Push Mobile, Rugambo Rodney (kushoto) akimkabidhi
funguo za magari mawili, Diana Elis Mkoba, baada ya kushinda shindano la
Tamasha la Serengeti Fiesta 2012. Diana alikabidhiwa magari mawili aina
ya Vitz yenye thamani ya shs milioni 18.Katikati ni Baba mdogo wa mshindi, Gratian Mkoba ambaye ni Rais wa chama cha Walimu Tanzania (CWT).
Mshindi wa magari
mawili yaliyotolewa na kampumi ya Push Mobile kwa ajili ya tamasha la
Serengeti Fiesta, Diana Elis Mkoba, akiwa ndani ya moja ya gari
alizozawadiwa baada ya kushinda bahati nasibu hiyo. Picha na Mpiga Picha Wetu
******************************************
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya Push Mobile imemkabidhi, Diana Elisa Mkoba, Magari mawili aina ya Vitz yenye
thamani ya sh. million 16 kufuatia promosheni iliyoendeshwa wakati wa
tamasha la Fiesta katika mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara.
Magari
hayo yalikabidhiwa na Meneja Mauzo na Masoko wa Push Mobile, Rodney
Rugambo katika hafla fupi iliyofanyika jijini, Dar es Salaam leo.
Rugambo
alisema kuwa wamefarijika kuwa wadhamini wasaidizi wa tamasha hilo
lililodhaminiwa na bia ya Serengeti kutokana na kutoa mchango wao katika
jamii, hasa kwa kupitia muziki wa kizazi kipya.
Alisema
kuwa zawadi hiyo ya magari mawili ni itimisho la magari sita waliyotoa
katika mikoa mbali mbali wakati wa tamasha hilo. Kampuni hiyo ilitoa
gari moja moja mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya, Mwanza na Dodoma.
Mbali
ya zawadi hizo, kampuni hiyo pia ilitoa zawadi ya pikipiki 15, simu ya
mkononi aina ya Nokia dabodabo 130, simu aina ya blackbey 14 na washindi
wa fedha taslim shs milioni 20. Thamani ya vitu vyote hivyo ni milioni
200.
“Ni
matarajio yetu kuwa Diana atayatumia magari haya ipasavyo na
tunampongeza kwa ushindi, watu wengi walishiriki katika bahati nasibu
hii na Diana kubahatika kushinda magari mawili, tunawaomba wadau
washiriki katika promosheni zetu nyingine,” alisema Rodney.
Diana alisema kuwa amefurahi kushinda zawadi hiyo kwani hakuamini baada ya kupokea simu ya ushindi wa zawadi hizo. Alisema
kuwa kwa vile yeye ni mwanafunzi wa chuo cha Bandari atatumia gari moja
na lingine atajua wapi kulipeleka, kama Kagera kwa mama yake au libaki
hapa hapa Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)