Mtu mzima Rick Ross “The Boss”
kutoka nchini Marekani hivi sasa yuko jukwaani kwenye Tamasha la
Serengeti Fiesta 2012 linalofanyika kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni
jijini Dar salaam ,anakamua ile mbaya na mashabiki wamepagawa
vyakutosha kwa kila anachowaelekeza kufuata wanafuata jamaa amefunika
mbaya, hiii ni mara yake ya kwanza kufanya onesho nchini Tanzania
Rachel Mwanamuziki wa
Bongofleva kutoka kundi la THT akicheza na mmoja wa wacheza shoo wake
katika Tamasha la Serengeti Fiesta linalofanyika usiku kuu kwenye
viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam ambapo pamoja na wasanii
mbalimbali wakali wa nyumbani, mwanamuziki maarufu wa Hiphop kutoka
nchini Marekani Rick Ross “The Boss” atahitimisha tamasha hilo kwa shoo
kali usiku huu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)