ONESMO NGOWI AMUOMBA RADHI IMANI MAKONGORO, GAZETI LA MWANANCHI NA WASOMAJI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

ONESMO NGOWI AMUOMBA RADHI IMANI MAKONGORO, GAZETI LA MWANANCHI NA WASOMAJI

DAR ES SALAAM, Tanzania
RAIS wa TPBC, IBF, AMEAPG, ECAPBA, Onesmo Ngowi (pichani kushoto), amemuomba radhi mwandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications – inayochapicha magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen, Imani Makongoro kwa kile alichokiita ‘Umbumbumbu’ wa mwandishi huyo.

Katika taarifa aliyoitoa mapema leo, Ngowi chini ya kichwa cha habari: “Umbumbumbu wa Imani Makongoro mwandishi wa gazeti la Mwananchi,” alikosoa kile kilichoandikwa na mwandishio huyo kwenye gazeti la Mwananchi, huku akitishia kumfikisha mahakamani kwa kumchafulia jina.

Lakini hivi punde, Ngowi amefuta kauli na kusudio lake kwa Makongoro, hii ikiwa ni kwa mujibu wa taarifa ya pili aliyoitoa jioni hii kwa vyombo vya habari. Ifuatayo ndio taarifa kamili kama ilivyoandikwa na mwenyewe Ngowi. Fuatilia taarifa yake hapa chini...........

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
OCTOBA 22, 2012

“Leo hii nilituma taarifa ambayo ilijaribu kuijibu makala iliyoandikwa na "Imani Makongoro" mwandishi mwandamizi wa gazeti la Mwananchi.

Taarifa hiyo ya Makongoro iliyokuwa na kichwa cha habari “Umbumbumbu wa Imani Makongoro mwandishi wa gazeti la Mwananchi” ilitumwa kwenye vyombo vya habari leo hii!

Nataka kuchukua fursa hii kuifuta taarifa hiyo na kuwaomba radhi Imani Makongoro, gazeti la Mwananchi pamoja na wasomaji wote walioipata na kusumbuliwa na taarifa hiyo!

Nafanya hivi nikijua kuwa taarifa yenyewe ilitoka kabla ya kushauriana na washauri wangu. Naamini kuwa uandishi wa habari ni wito na unafanyika katika mazingira magumu sana hapa Tanzania.

Mimi sina nia ya kuisema wala kuikandamiza taaaluma ya uandishi wa habari. Aidha sina haja ya kuwafanya waandishi wa habari wasiandike yale wanayofikiri kuwa ni mema kwa jamii!

Ndiyo maana nachukua fursa hii kumuomba radhi Imani Makongoro, Gazeti la Mwananchi pamoja na wote waliopata taarifa ile kwa usumbufu walioupata.

SAMAHANINI SANA!!!

Imeandikwa na:
Onesmo Ngowi
Rais wa,TPBC, IBF AMEAPG, ECAPBA
Mkurugenzi CBC

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages